Hotuba ya Mugabe Addis imeibua mawazo kinzani: Je kafanya nini akiwa kama mwenyekiti wa AU?

February 3, 2016 § 2 Comments

Hotuba ya Rais Robert Mugabe kule Addis wakati wa kumaliza kikao cha viongozi wa Afrika imevuta hisia mchanganyiko kwa watu mbali mbali. wengine tumefurahia kuona Mugabe bado ana ujasiri wa kuwakandia wazungu. Wengine tuna “reservations”. Nikaona ni vizuri nitoe maoni yangu. Mengi nimeshayasema kwenye kurasa za marafiki zangu lakini nimeonelea niyakusanye na kuyaweka hapa pamoja pia.

Mwanzoni niliposikia hotuba ile nilipatwa na mawazo mchanganyiko mawili. Kwanza niliona yes Mugabe ni shujaa anaweza kusema ukweli kama ulivyo. Ikiambatana na hilo nikaona pia kudai kiti katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni haki yetu na kuomba Umoja wa mataifa ufanyiwe matengenezo (reforms) ni sahihi. Upande mwingine ukanishawishi kuangalia record ya mzee Mugabe na kulinganisha na ukali wa maneno yake juu ya nchi za magharibi zilizokuwa zikimtaka atoke madarakani. Nikaona picha pia ya jinsi uongozi ng’ang’anizi ulivyoiletea madhara nchi yake. Nikasikia pia alivyomsifia Mwalimu na mchango wake katika ukombozi wa Afrika akitahadhari kuzungumza upana wa falsafa za Mwalimu. Nikagundua kuna tatizo kubwa kwa Mugabe na Afrika yetu.

Kuna watu tunafurahia sana lugha za kutukana wengine tukisikia mtu anatukanwa na hasa mzungu tunafurahi sana. Kwa kanuni aliyotufundisha Mwalimu hotuba ya Mugabe kule Addis haikuwa nzuri. Kutumia kauli za kibaguzi kama “white faces na pink noses” kwa maoni yangu si mujarabu hata kidogo. Na hatupaswi kushangilia. Sisi tuliwachukia wakoloni si kwa sababu ya rangi yao bali kwa vitendo vyao. hatupaswi kabisa kulipiza kwa kauli za kibaguzi namna ile. Baraza la usalama halina wazungu peke yake wako wachina pia. Alipogundua kwamba yuko Ban Ki Moon pale akaanza kubadili kauli jambo ambalo ni unafiki. Lakini kwa sababu aliyetukanwa ni mzungu tunafurahia. vitendo anavyowafanyia wazimbabwe si vizuri na kiburi anachowajengea viongozi wa Afrika cha kung’ang’ania madarakani si jambo jema kwa bara letu.

Anamsifia Nyerere lakini hataki kuishi kanuni zake. Mugabe ni hatari kwa Afrika. Alikuwa amejiwekea rekodi nzuri lakini yote kaiharibu hafai kuigwa. Kupigania kiti kwenye Baraza la Umoja wa mataifa hakusaidii chochote Afrika isiyokuwa na umoja, isiyoweza kutatua matatizo yake yenyewe. Afrika inatakiwa kwanza itengeneze sauti yake, ikisema kitu dunia ielewe Afrika imesema. Afrika imeshindwa hata kutengenza umoja imara wa kikanda. Afrika bado inaamini katika vinchi vidogo vidogo ambavyo ni vichaka vya madikteta wanaokutana Addis na kufanya matamko yaliyojaa hewa tupu hayana madhara. Badala ya kuendelea kuwaaminisha watu kwamba matatizo yetu si kwa sababu yetu wenyewe na viongozi wetu Mugabe anataka tuamini kuwa matatizo yetu ni kwa sababu hatuna kiti katika baraza la usalama la umoja wa mataifa ni upuuzi uliopitiliza.

Kuna damu za waafrika zinamwagika Burundi, DRC, CAR, Libya, Somalia na shida ya Boko Haram Nigeria ilyosambaa kwa majirani wote. AU imeyafanyia nini? Kama mwenyekiti wa AU Mugabe kasaidia kitu gani Burundi? Hivi kati ya suala la Burundi na kesi ya kina Ruto kule ICC kipi ni muhimu zaidi kwa Afrika? Kinachoendelea Burundi ni dhahiri kuwa Warundi wenyewe hawataweza kuutatua ule mgogoro. Nkurunzinza na wenzake walioko madarakani wataendelea kuua wapinzani. Leo Tanzania tuna wakimbizi zaidi ya laki moja kutoka Burundi kwa sababu ambazo Afrika ingeweza kuzuia. Mugabe ame-deliver nini katika term yake kama mwenyekiti wa Afrika? Viongozi wanatumia kodi zetu kusafiri na kukutana Addis kufanya nini cha mno ambacho kina mguso kwetu?

Katika mojawapo ya hotuba za Mwalimu akiwa kiongozi wa Tume ya kusini (South – south Commission) alisema wazi kuwa kizazi cha pili cha viongozi wa Afrika kilikuwa na jukumu la kuleta umoja wa Afrika ili bara la Afrika liwe na sauti moja duniani. Alisema tukiwa na sauti moja tuna nafasi nzuri ya kusikilizwa. Sasa tangu Mwalimu aliposema tumekuwa na vizazi (vya uongozi) vitatu na hiki sasa cha nne njozi ya umoja iko mbali hata kuliko wakati wa waasisi wa wa Afrika (kina Kwameh Nkurumah, Julius Nyerere, Jomo Kenyatta, Haile Selasie, Gamal Abdel Nasser, nk) mwaka 1963. Nikiwa Darasa la tano Mwaka 1981 ndipo African Economic Community (Jumuia ya uchumi ya Afrika). Leo ukiwazungumzia kizazi cha sasa wanakushangaa! Bado waafrika tunatumia passport kwenda nchi nyingine, ukikutwa nchi nyingine bila “makaratasi” unafukuzwa, huu uchumi wa pamoja itakuwaje? Ni nini kinatuzuia Africa kuwa shirikisho lenye nguvu la kiuchumi? Halafu leo nimsifie Mugabe kwa maneno rahisi ya kutafuta umaarufu kwa wasikilizaji? Hapana?

Wanaume tulofikisha miaka 40 tupime tezi dume tuache kujazana ujinga

January 30, 2016 § Leave a comment

Nimeona watu wanafanya mzaha juu njia ya kupima ukuaji wa tezi dume iitwayo DRE (Digital Rectal Examination) Tukumbumbuke tu kwamba si kila kukua Kwa tezi dume ni kansa. Kuna ile madaktari wanaita Benign Prostate Hyperplasia. Kuna dawa ya ku-control kwa sababu ikikua huminya kibofu Na kufanya uende haja ndogo mara Kwa mara. Niwasihi sana wanaume tuache myths za kijinga Na uoga usio Na maana. Matatizo ya tezi dume yakigundulika mapema hutibika. Kama mtu kafikisha miaka 40 Ni muhimu akapime na baada ya hapo daktari atakushauri uwe unapima kila baada ya muda gani.

Kuna njia tatu ninazozifahamu Za kupima tezi dume, tuzipitie kama nilivyozinukuu: 
1. PSA blood test (nimeshafanya kipimo hiki ikiambatana Na cha ultrasound)
Maelezo kutoka UK Cancer research test ni Haya:

PSA is a protein produced by both normal and cancerous prostate cells. A high level of PSA can be a sign of cancer. But your PSA level can also be raised in prostate conditions that are not cancer (are benign) or if you have an infection. To check for PSA (prostate specific antigen), your doctor takes a sample of your blood. Your doctor may want to rule out a urine infection before carrying out a test. If you’ve had a urine infection, you shouldn’t have a PSA test for at least a month after your treatment finishes. 
PSA is usually measured in nanograms per millilitre of blood (ng/ml). There is no one PSA reading that is considered normal. The reading varies from man to man and the normal level increases as you get older. But the following values are a rough guide
3 ng/ml or less is considered to be in the normal range for a man under 60 years old
4 ng/ml or less is normal for a man aged 60 to 69

5 ng/ml or less is normal if you are aged over 70.

A reading higher than these values but less than 10 ng/ml is usually due to a non cancerous (benign) enlargement of the prostate gland. A reading higher than 10 ng/ml may also be caused by benign prostate disease, but the higher the level of PSA, the more likely it is to be cancer. Sometimes a cancer may be diagnosed in a man with a PSA reading within the normal range. But usually, the higher the reading, the more likely it is to be cancer. 

Some men have PSA levels in the hundreds (or even thousands) when they are diagnosed. The higher the level of PSA at diagnosis, the more likely the cancer is to spread quickly.
PSA blood tests are also used to monitor how well prostate cancer treatment works or to decide whether you need treatment. If your PSA is stable, it is a sign that a cancer is not growing or spreading. Successful treatment shrinks cancer and so the PSA level in the blood then falls.
2. Rectal examination (nadhani ndo wanaume tunachokiogopa)
Maelezo yake kutoka chanzo kilekile Ni Haya:
Your doctor puts a gloved finger into your back passage (rectum) to feel your prostate gland and check for abnormal signs, such as a lumpy, hard prostate. Doctors call this test a digital rectal examination (DRE).
Mchoro unaonyesha tezi dume ilipo nimeambatanisha. Ukiangalia huo mchoro uatajua Kwa nini madaktari hutumia njia hii ya DRE (Digital Rectal Examination) kupima.
  
3. Rectal ultrasound (hii hasa ni kuchunguza tezi dume kitu Kama ukubwa wake)
You may have a rectal ultrasound scan to examine the prostate gland. It is called a trans rectal ultrasound (TRUS). You will need to make sure you have had a bowel movement beforehand so that your rectum is empty when you go for your appointment. 
Your doctor puts a small ultrasound device into your back passage. It produces sound waves to create a clear picture of the prostate gland. This test is uncomfortable, but shouldn’t hurt. It does not take long.

Neno gani unachagua kulitumia mwaka 2016 kukutia moyo kuleta tofauti (which one word you choose to use in 2016 to motivate yourself)

January 5, 2016 § Leave a comment

Psychologists tell us that words can create, find one key word which you will use in 2016 to motivate you to succeed in what you do! And please feel free to share your one word with us. You don’t need to justify, just say it. Do not be in hurry to say it for the sake that you’ve said it, it isn’t a competition or test. Give it time by experimenting it, it may take a day or a week but surely not a month. If it takes you more than a week you probably need some help. 
Please share this message to your friends so that we can encourage each other to make a difference in our lives. 

Wataalamu wa saikolojia wanatuambia maneno huumba. Tafuta neno moja tu utakalokuwa ukilitumia mwaka 2016 kukupa nguvu ya kufanikiwa shughuli zako! Tafadhali jisikie huru kushiriki nasi hilo neno lako. Huna haja ya kulielezea litaje tu inatosha. Pata Muda wa kutosha kulitafakari na kulijaribisha, yaweza kukuchukua siku au wiki lakini si mwezi. Ikikugharimu zaidi ya wiki kupata hilo neno utakuwa na shida mahali fulani na utahitaji msaada. 

Wapatie huu ujumbe marafiki zako pia tushiriki pamoja kutiana moyo kuleta tofauti katika maisha yetu.

Salamu na nasaha za mwaka 2016 Kwa ndugu, jamaa na marafiki zangu wote

January 1, 2016 § Leave a comment

Ndugu wapendwa wote nimeguswa sana na ushirikiano wenu katika mijadala mbalimbali kupitia hii teknolojia kwa mwaka ulopita, Niwatakie heri na fanaka kwa mwaka 2016. 
Niwaombe tu mwaka huu kila mmoja wetu ajaribu kupiga hatua moja au zaidi kusogelea malengo yake. Tusione shida kubadili njia ya kufikia malengo yetu kama ile nyingine itashindikana. Tusing’ang’ane kwenye aina moja ya kazi Kama haina mabadiliko. Mfano kama hupandi ngazi katika ajira uliyo nayo Kwa miaka kadhaa sasa move on. Usigeuze mwajiri kuwa baba au mama. Jari sana afya yako usipakize uchafu mwilini mwako. Sema Kwa sigara na pombe basi, usiwe mtumwa kwavyo. Anza kuwaaga marafiki ambao hawakuongezei kitu mfano mwaka huu hawakukushauri kitu chochote cha maana. Usiwe mvumilivu kupita kiasi Kama unakerwa na jambo sema wazi usinung’unike pembeni. 

Kwa wale ambao hamjaoa wala kuolewa usioe au usiolewe na mtu kabla hamjagombana kwa jambo fulani. Ni vizuri mahusiano yenu yakajaribiwa muone mnapitaje hapo. Ndoa ni Kama barua iliyoko ndani ya bahasha hutajua kilichomo hadi ufungue na kusoma. Ndoa kamili haifungwi pale unaposema “I do”. Ndoa nyingi zimekuja kufungwa kikamilifu na kiuhalisia baada ya miaka kadhaa. Upendo si kipofu usijifanye kipofu Kama unaona jambo ambalo linakukera Kwa mchumba wako usijidanganye eti akinioa au nikimwoa atabadilika. Uzoefu mwingi umeonyesha ukimuoa au akikuoa tatizo litakuwa kubwa zaidi. Lakini kumbuka ndoa hutengenezwa na binadamu kubali ku-adjust pale unapoweza.

Mwaka 2016 unagawika kwa nne hautatokea mwaka wa namna hii tena hadi baada ya miaka 3. Rafiki alozaliwa Tarehe 29 mwezi wa pili atasherekea birthday yake mwaka huu na hongera sana. Baada ya hapo hatasherehekea siku yake ya kuzaliwa hadi mwaka 2020! Wale tunaosherehekea birthday zetu kila mwaka tunachukulia poa sana. Tujue kuna mambo Na nafasi zingine tukizizubalia itachukua muda kujirudia au inaweza isitokee tena. Tujifunze kuiishi siku Kwa ukamilifu wake (live the day to the fullest)

Niwatakie tena heri Na fanaka tele Kwa mwaka 2016!

Kulipa kodi Na kusimamia matumizi yake Ni wajibu wa kila Mtanzania

December 23, 2015 § Leave a comment

Nimebahatika week hizi mbili kuwa site agent- kusimamia ujenzi mahali fulani. Kazi hii imenipa nafasi ya kutembelea maduka kadhaa ya wafanya biashara. Nimegundua mambo yafuatayo:
1.Wauza bidhaa pamoja na kuwa na Mashine za EFD za kutoa risiti za mauzo ili mamlaka husika ziweze kujua ni sehemu gani ya mauzo inatakiwa kutozwa kodi, hawafurahii kutoa risiti. 

2. Ukiwataka watoe risiti wanakwambia mtandao uko na shida. Kwa sababu nina uelewa wa mambo ya IT mmoja nikamwambia anipe nijaribu kuona na kusaidia, alikataa. 

3.Ukidai risiti wanapandisha bei mlopatana mwanzo. Risiti inakuwa adhabu kwa mteja hivyo kufisha moyo mteja kang’ang’ania risiti 

4.Bei kwenye maduka hazibandikwi ili kulinda haki za mlaji. Hii inawapa wafanya biashara uwanja mkubwa wa kucheza na saikolojia ya mlaji. Hii sijawahi kuiona nchi zilizoendelea ambazo serikali zake zinawajibika kwa wananchi. Bei ni Lazima zibandikwe kwa kila bidhaa. 

5.Nilienda Sao Hill pia pamoja na shughuli zangu nilitaka kujua kwa nini wanashindwa kuiuzia au kuitosheleza Tanesco na nguzo za umeme ili hali wana miti ya kutosha. Nilichoambiwa kiliniacha midomo wazi. Sitakisema kwa sasa. Ila nashangaa serikali yenye mikono mirefu inashindwaje kushughulika na jambo hili once and for all ili kuleta nidhamu katika taratibu za manunuzi. 

Nashauri tu wananchi kama kweli sauti ninazozisikia mtaani ni za dhati kutoka kwenye mioyo ya Watanzania kwamba, “tumepata jembe”, “Rais huyu ndiye tuliyemtaka”, “Kama akiendelea hivi…”, “tunamkubali ” na maneno mengine mengi, tumsaidie huyu ndugu yetu. Tufanye wajibu wetu. Mfano kama sote tukiamka leo tunaokwenda madukani tuwaambie wafanya biashara hakitaeleweka hadi watupe risiti, mbona nchi itapata adabu kwa ghafla!

Matatizo ya Tanesco: Je, Kama Nchi Tuna nia ya Dhati ya Kuyatatua?

December 5, 2015 § Leave a comment

Nimekuwa Na maswali machache baada ya kusoma habari ya Jana kuhusu Tanesco kutoka Kwa gazeti la Daily News isemayo, “Tanesco in Financial Mess”.  

Bila kujali tofauti zetu kisiasa hivi Tuna Tatizo gani na kuendesha mashirika ya umma?
Najua kuna madeni makubwa serikali na   taasisi zake zinadaiwa iweje watu maskini kuliko serikali tanaweza kulipia bili zetu tena hata kabla ya kutumia huku umeme ukikatwa ovyo ilihali serikali ambayo taasisi zake hata kukiwa na mgao zenyewe zinaendelea kupata umeme kama kawa Na hazilipi?

Je, inawezekana serikali inafanya makusudi ili kuiua Tanesco Kisha wapate sababu ya kuiuza Kwa wageni? Kwa nini inashindwa kulipa?

Kwa uongozi wa Tanesco: hivi Tanesco iko huru kupanga mikakati yake na kisha mpango biashara na namna ya kujiendesha kwa faida bila kuingiliwa? Hii mikataba ya songas na mingine ya uzalishaji na kuiuzia Tanesco inawezekana kibiashara na kiuchumi (is it a viable business case? Maana katika biashara kuna kitu tunaita uendelevu wa biashara na wateja wako yaani business sustainability au tulivyozoea sustainable development. Yaani tunapofanya biashara na mtu hatufanyi Kwa gharama ya kesho yaani kana kwamba kesho hapatakuwa na kizazi kingine cha kufanya nacho biashara. Tunaita biashara ya kuua.

Je wanaoiuzia umeme Tanesco wanajali pia kuna kesho? Au Ni leo tu yaani Chukua Chako Mapema maana kesho si yako? Kanuni nzuri ya biashara endelevu Ni kwamba huchukui faida kubwa kiasi cha kuathiri ulinganifu wa biashara kesho.

Mwaka 85 nilipogoma kubeba bango kwenye sherehe Za wafanyakazi, nakumbuka kwenye hotuba yake Mwalimu alisema mabepari Ni sawa na majibwa ukiyatupia chakula hugombania, je Kwa muktadha huu Tanesco imetupiwa Haya majamaa wanaigombania?
Deni wanalodai Songas la miezi 14 ni Dola milioni 100 sawa shs zetu 200,000,000,000 sawa na bilioni 200! Sawa na bilioni 14 na milioni 300 kila mwezi. Yaani milion 1,000 mara 14 halafu kana kwamba haitoshi unaongezea million zingine 300. Hapo bado IPTL na mtoto yule wa Richmond (Dowans)! 
Tujadili wenye nafasi!

Ni wakati wa kutafakari na kufanya maamuzi sahihi: Kwa miaka 38 tumekuwa nchi ya kauli mbiu kila baada ya miaka 5

September 25, 2015 § Leave a comment

Ethiopia wamezindua treni ya umeme ninachojua ni ya kwanza kwa East, central Africa na Southern Africa (ukitoa South AFrica) (sijui West na North Africa kama wana treni ya namna hiyo) Nilikuwa Ethiopia mara ya kwanza mwaka 2003 na mara ya mwisho mwaka 2009. 2009 nilikuta wamemaliza:

– kujenga ile ring road na sasa hivi treni ya umeme!

– Njaa iliyokuwa inatesa nchi ni historia!

– Kahawa wanaongoza sasa!

– Viwanda vidogo vimeshakua na vinazalisha kwa masoko ya nje
pia mfano viatu!

– Shirika lao la ndege ni kubwa kuliko mashirika yote ya ndege
Africa!

– Kazi ya kujenga bwawa kubwa la Hidase la kuzalisha umeme wa MW 6,000
litakalokuwa la 11 kwa ukubwa duniani na linajengwa kwa fedha za ndani,
ujenzi umefikia kiwango cha zaidi ya %50 sasa! n.k

Hiyo ndiyo tofauti kati ya inchi inayoongozwa na watu wa vitendo na nchi inayoongozwa na watu wa longolongo. Kama raia wa nchi hii nina siku kadhaa za kufikiria na kuamua. Ili tusonge inaonekana itabidi tuachane na upenzi huu tulete mabadiliko na siyo marekebisho tu. Logic inaanza kunituma kuwa huwezi kulisukuma gari bovu ukiwa ndani, ni lazima utoke nje. Inaonekana tarehe 25 October mwaka huu nitashauri Watanzania wote bila kujali itikadi tulizokuwa nazo na upenzi tutoke kwenye hili gari tulisukume. Ninampenda sana Dr Magufuli lakini naipenda zaidi nchi yangu. Tunataka sasa Tanzania nyingine ambayo viongozi tuliowapa dhamana kila kukicha watakuwa wanatafuta sababu kwa nini jambo fulani lisifanyike na si kutumia muda na mali zetu kutafuta sababu za kuelezea kwenye majukwaa kwa nini halikufanyika.

Mungu ibariki Tanzania!

Mungu ibariki Africa