Kuwa chini ya sheria ni sawa na kuwa na simu “feki” ambayo kila wakati unahofu kuwa TCRA wataizima

June 21, 2016 § Leave a comment

Kuwa chini ya sheria ni sawa na kuwa na simu “feki” ambayo kila wakati unahofu kuwa TCRA wataizima. Kuishi katika neema ya Kristo ni sawa na kuwa na simu “original” hata siku ya kuzima simu feki wewe hutaona chochote katika simu yako. Utakuwa unaendelea ku-whatsapp kama kawaida!

Katika neno la Mungu Mtume Paulo kazungumza changamoto za kuishi maisha ya utii na kusema wazi kuwa tukimwamini Kristo hatuko chini ya sheria. Kuna watu huwa hawaelewi wanafikiria kutokuwa chini ya sheria basi ni kuvunja sheria na kutokuwa waangalifu wa kufuata taratibu iwe za kiroho (moral laws – Amri kumi za Mungu Kutoka 20:1-17 ambazo zimegawika sehemu mbili ya kwanza: Amri ya 1 – 4 Upendo kwa Mungu aliyetuumba na sehemu ya pili Amri ya 5 – 10 Upendo na mahusiano na binadamu wenzetu), kimwili kama sheria za afya (health principles) au sheria za nchi (civil laws). Dhamira ya hatia hutusumbua kwa sababu ya kuvunja sheria au kuishi kinyume na taratibu na kanuni. Kuondokana na hiyo ni bora kumwamini Yesu na kumtegemea maana yeye husamehe makosa na kuyafuta kisha hutuwezesha sasa kuishi ndani ya utii.

Leo nizumguzie sehemu ya sheria za afya. Wengi leo tuna madhira makubwa kimwili kwa sababu ya kutokuheshimu sheria za afya. Mfano ulaji (tule nini), Unywaji (tunywe nini), Hewa (tuvute hewa yanamna gani) na kadhalika. Kuna baadhi yetu tumegeuza miili yetu kuwa madampo. Tunapakiza kila aina ya uchungu ndani ya miili yetu. Katika kitabu cha Mambo ya Walawi sura ya 11, Mungu aliwapa wanadamu sheria za ulaji. Ujue binadamu wa mwanzo walikuwa hawali nyama. imekuja kuruhusiwa baada ya gharika. Hata hivyo Mungu aliweka utaratibu wanyama wapi wa kuliwa na wapi si wakuliwa. Tuache ubishi. Tena tukiweza tuache tu kula nyama maana haikuwa katika mpango wa Mungu Tangu alipotuumba.

Sigara, mirungi, madawa ya kulevya, bangi, pombe na jamii yake tutafakari na kufanyia mazoezi ya kuacha kutumi vitu hivyo vina madhara makubwa si katika afya zetu tu bali hata kwa afya ya familia na jamii kwa ujumla. Kuna ubishi mwingi na sarakasi kwenye haya lakini uchaguzi wa kuacha ni salama kwetu. Kuna kijitabu nilikisoma zamani, kinaitwa, “Watumwa Wangali hata Leo”. Kinasema utumwa si tu ule wa zamani au kikoloni. Kuwa mfungwa wa kutumia vitu (addiction) ni ka aina ka utumwa kabaya sana. Kuna watu wanahangaika kutoka kwenye utumwa huu, wana nia ya kuacha lakini imeshindikana. Niwape matumaini kuwa inawezekana. Mzee mmoja rafiki yangu ni raia wa nchi fulani ambapo uvutaji wa sigara umetamalaki kupita maelezo. Nikajaribu kumuuliza kama anajua madhara ya sigara, akasema anayajua na ilishamharibu koo akafanyiwa upasuaji. Lakini akaniambia ndiyo starehe ilyobaki hawezi kuacha mpaka kufa. Huyu ni tofauti na wengi wengine wetu. Wengi hawajui madhara ya sigareti. Tumeweka utaratibu katika matangazo ya sigara kwamba ina madhara kwa afya yako. Maandishi haya hayaeleweki maana yake nini hasa kwa watumiaji. Tataendelea kuweka msukumo kwa viwanda hivi hatari vifungwe kuokoa maisha ya watu wetu.

Ulaji wa mbovu: unaweza kuwa unakula kuzingatia kanuni za nini ule lakini hufuati utaratibu mzuri wa kula. Hii nayo ni hatari. Kuna watu wanakula ovyo ovyo. Akiona kitu hata barabarani udenda unamtoka. Kanywa chai, Kala mchana na hata usiku. Lakini anataka ale pia katikati, akiona tukaranga huyo, korosho hazimpiti, Vitumbua anavyo, maandazi ooohhhh!, Juice za Azam barabarani hazikatishi mbele yake. Mikia ya pweza yumo. Akiona mtu anapitisha tumhogo atataka hata kakipande kadogo tu. Keki hazipiti, sijui aiskrim, popcorn, tuvikombe twa kahawa barabarani na vingine vingi, havikatishi mbele ya macho yake. Hii ni hatari. Kwanza unaweza kula vitu ambavyo haviko katika usafi (ukaambukizwa magonjwa), pia tumbo linahitaji muda wa kusaga chakula ulichokula ama asubuhi au mchana au jioni. Tujiepushe na kula katikati ya milo. Tuna shida ya mila na desturi pia, mtu akija kwako akikwambia kashiba usimlazimishe eti akuachie baraka – yeye unamwachia laana. Tunywe maji ya kutosha (walau lita mbili) kwa siku. Kuna watu asubuhi hadi jioni hanywi maji halafu anajisifia ka zuzu, “mie naweza kwenda hata siku mbili bila kunywa maji”, ole wako. Kunywa maji nusu saa kabla au baada ya kula, usinywe maji huku unakula chakula unaharibu na kuchelewesha mfumo wa kusaga chakula.

Chakula kiwe kamili (balanced diet) vyakula vya kukinga mwili, kuleta joto na kujenga mwili. Usikoboe nafaka mfano mahindi. Yasage hivyo hivyo. Kwa nini uzidiwe akili na wadudu na panya? Wakila mahindi wao hula kiini cha hindi. Maganda yanayozunguka hindi ni ufagio tumboni mwako. Kula vyakula vyenye jamii ya mifagio mfano mboga za majani nyingi. Usione ufahari kukaa muda mrefu bila kwenda haja kubwa. Hiyo ni hatari!

Leo niishie hapa kwa afya: Tukitii kanuni za afya itakuwa sawa na kuwa na simu original wewe utayeya tu na mawasiliano. Ukiendekeza kuvunja kanuni za afya utakatwa kama yule jamaa yangu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

What’s this?

You are currently reading Kuwa chini ya sheria ni sawa na kuwa na simu “feki” ambayo kila wakati unahofu kuwa TCRA wataizima at kadulyu.

meta

%d bloggers like this: