Je, mitambo ya kusindika vyakula Tanzania inatumia “food grade lubricants”?
March 6, 2016 § 2 Comments
Jana nilikuwa na rafiki yangu anayehusika na mambo ya viwango tukazungumza mambo kadhaa kuhusu viwango vya bidhaa mbalimbali hapa nchini. Kuna wakati niliwahi kurusha kwenye mtandao mwingine juu ubora wa nondo tunazojengea hapa nchini baada ya kuzifanyia majaribio binafsi. Bahati mbaya kabisa viongozi wetu wa mashirika kama TBS au taasisi kwa ujumla ama hawako au hawashiriki kwa mitandao ya jamii. Nashauri wafanye hivyo ili tusaidiane na umma kuibua matatizo ya viwango.
Tanzania tuna viwanda vya kusindika vyakula na madawa kwa ajili ya matumizi ya wanadamu na mifugo ambayo wengi wetu huila pia au kutumia mazao yake kama maziwa nk. Tukiwa na mjadala na huyu ndg yangu nikaibua hoja ya vilainishi vya mitambo inayosindika vyakula. Katika mitambo hiyo Kuna sehemu tunaita nyeti (critical areas) ambapo chakula kinaweza kutana na vilainishi kiuhalisia kulinda afya ya binadamu nchi zilizoendelea zimeamua tu kwamba mtambo unaosindika vyakula wote ni critical. Hivyo ni lazima kutumia “food grade lubricants” mazao ya plastic zinazotumika kubeba chakula na maji ni lazima ziwe food grade pia.
Sasa swali: je, viwanda vyetu vinavyozalisha chakula vinatumia food grade lubricants kuepusha uchafuzi wa chakula? Nani anahakikisha hilo linafanyika? Total food grade policy Inatokana na ukweli kwamba mafundi wanaweza kuchanganganya lubricants hivyo kuondoa huo uwezekano ni kutumia food grades kwa mitambo yote ya kusindika vyakula. Na watu wasitoe sababu, kwenye soko tuna hydraulic oil, transmission oil, greases za food grade.
Tujilinde wapendwa na wenye mandate hiyo ni TBS na TFDA.
Huu mradi ni muhimu jinafasi uuanzee nitakusaidia
Hi Geofrey,
Asante tutafutane. Food grades inabidi kwanza ziwe enforced na TFDA ni muhimu kucheck wana sera gani. TBS nilishacheck nao hakuna kitu pale.
Regards,
Kadulyu