Kulipa kodi Na kusimamia matumizi yake Ni wajibu wa kila Mtanzania

December 23, 2015 § Leave a comment

Nimebahatika week hizi mbili kuwa site agent- kusimamia ujenzi mahali fulani. Kazi hii imenipa nafasi ya kutembelea maduka kadhaa ya wafanya biashara. Nimegundua mambo yafuatayo:
1.Wauza bidhaa pamoja na kuwa na Mashine za EFD za kutoa risiti za mauzo ili mamlaka husika ziweze kujua ni sehemu gani ya mauzo inatakiwa kutozwa kodi, hawafurahii kutoa risiti. 

2. Ukiwataka watoe risiti wanakwambia mtandao uko na shida. Kwa sababu nina uelewa wa mambo ya IT mmoja nikamwambia anipe nijaribu kuona na kusaidia, alikataa. 

3.Ukidai risiti wanapandisha bei mlopatana mwanzo. Risiti inakuwa adhabu kwa mteja hivyo kufisha moyo mteja kang’ang’ania risiti 

4.Bei kwenye maduka hazibandikwi ili kulinda haki za mlaji. Hii inawapa wafanya biashara uwanja mkubwa wa kucheza na saikolojia ya mlaji. Hii sijawahi kuiona nchi zilizoendelea ambazo serikali zake zinawajibika kwa wananchi. Bei ni Lazima zibandikwe kwa kila bidhaa. 

5.Nilienda Sao Hill pia pamoja na shughuli zangu nilitaka kujua kwa nini wanashindwa kuiuzia au kuitosheleza Tanesco na nguzo za umeme ili hali wana miti ya kutosha. Nilichoambiwa kiliniacha midomo wazi. Sitakisema kwa sasa. Ila nashangaa serikali yenye mikono mirefu inashindwaje kushughulika na jambo hili once and for all ili kuleta nidhamu katika taratibu za manunuzi. 

Nashauri tu wananchi kama kweli sauti ninazozisikia mtaani ni za dhati kutoka kwenye mioyo ya Watanzania kwamba, “tumepata jembe”, “Rais huyu ndiye tuliyemtaka”, “Kama akiendelea hivi…”, “tunamkubali ” na maneno mengine mengi, tumsaidie huyu ndugu yetu. Tufanye wajibu wetu. Mfano kama sote tukiamka leo tunaokwenda madukani tuwaambie wafanya biashara hakitaeleweka hadi watupe risiti, mbona nchi itapata adabu kwa ghafla!

Advertisements

Matatizo ya Tanesco: Je, Kama Nchi Tuna nia ya Dhati ya Kuyatatua?

December 5, 2015 § Leave a comment

Nimekuwa Na maswali machache baada ya kusoma habari ya Jana kuhusu Tanesco kutoka Kwa gazeti la Daily News isemayo, “Tanesco in Financial Mess”.  

Bila kujali tofauti zetu kisiasa hivi Tuna Tatizo gani na kuendesha mashirika ya umma?
Najua kuna madeni makubwa serikali na   taasisi zake zinadaiwa iweje watu maskini kuliko serikali tanaweza kulipia bili zetu tena hata kabla ya kutumia huku umeme ukikatwa ovyo ilihali serikali ambayo taasisi zake hata kukiwa na mgao zenyewe zinaendelea kupata umeme kama kawa Na hazilipi?

Je, inawezekana serikali inafanya makusudi ili kuiua Tanesco Kisha wapate sababu ya kuiuza Kwa wageni? Kwa nini inashindwa kulipa?

Kwa uongozi wa Tanesco: hivi Tanesco iko huru kupanga mikakati yake na kisha mpango biashara na namna ya kujiendesha kwa faida bila kuingiliwa? Hii mikataba ya songas na mingine ya uzalishaji na kuiuzia Tanesco inawezekana kibiashara na kiuchumi (is it a viable business case? Maana katika biashara kuna kitu tunaita uendelevu wa biashara na wateja wako yaani business sustainability au tulivyozoea sustainable development. Yaani tunapofanya biashara na mtu hatufanyi Kwa gharama ya kesho yaani kana kwamba kesho hapatakuwa na kizazi kingine cha kufanya nacho biashara. Tunaita biashara ya kuua.

Je wanaoiuzia umeme Tanesco wanajali pia kuna kesho? Au Ni leo tu yaani Chukua Chako Mapema maana kesho si yako? Kanuni nzuri ya biashara endelevu Ni kwamba huchukui faida kubwa kiasi cha kuathiri ulinganifu wa biashara kesho.

Mwaka 85 nilipogoma kubeba bango kwenye sherehe Za wafanyakazi, nakumbuka kwenye hotuba yake Mwalimu alisema mabepari Ni sawa na majibwa ukiyatupia chakula hugombania, je Kwa muktadha huu Tanesco imetupiwa Haya majamaa wanaigombania?
Deni wanalodai Songas la miezi 14 ni Dola milioni 100 sawa shs zetu 200,000,000,000 sawa na bilioni 200! Sawa na bilioni 14 na milioni 300 kila mwezi. Yaani milion 1,000 mara 14 halafu kana kwamba haitoshi unaongezea million zingine 300. Hapo bado IPTL na mtoto yule wa Richmond (Dowans)! 
Tujadili wenye nafasi!

Where Am I?

You are currently viewing the archives for December, 2015 at kadulyu.