Mabadiliko ni mchakato endelevu, yasipoleta tija kuna n’gwe ya pili, tatu nk

August 21, 2015 § Leave a comment

Baadhi ya Watanzania tunaotaka mabadiliko tunajichanganya. Tunazunguka mbuyu kwenye maoni yetu, tunaacha maswali badala kutoa majibu. Tunasema hatuna hakika tunataka mabadiliko gani halafu bado tunayataka. Tunasema hatuipendi CCM lakini tunaonyana tusiikatae hivihivi. Inachanganya sana kusoma maoni ya wadau wa mabadiliko kwa sasa. Kwa kawaida kabisa ukizungumzia mabadiliko ya kisiasa ni kubadili mfumo kutoka wa zamani kwenda mfuma mbadala (mpya). Bila shaka mabadiliko yoyote yaliyosubiriwa na jamii kwa muda mrefu hupokelewa kwa furaha bila kujali kesho patatokea nini. Idd Amin alipompindua Milton Obote, Waganda walilipuka kwa nderemo mitaani. Vivyo hivyo Kanu iliposhindwa Kenya, wakenya walifurahi sana (hata wale waliokuwa Kanu).

Consequences kwa mabadiko haya yalokuja kwa njia tofauti yalikuwa tofauti. Raia waliyafurahia na hiyo si dhambi. Kwa sababu watu wanapotaka mabadiliko maana yake kuna kitu hawaridhiki nacho. Kitakachotekea baadaye kama madhara ya mabadilko huwezi kuwalaumu watu kwa maamuzi waliyofanya bali mnaingia tena kwenye n’gwe ya pili ya mabadilko. Hakuna palipoandikwa kuwa mabadliko huwezi kuyabadilisha baadaye ukiona hayakuwa na tija. Ni kuwadanganya watanzania kuwashawishi kuwa mabadiliko watakayoyafanya sasa yateleta mbingu. Mabadiliko ni mchakato endelevu. Nikipima mambo yote kisiasa, kiuongozi, kiuchumi, huduma za jamii, utawala bora, bado naona ni wakati mwafaka wa Watanzania kubadili mfumo wa utawala wa sasa. Miaka zaidi ya hamsini imetosha. Kuna haja kabisa ya kubadili huu mfumo. Nimeanza kupiga kura tangu mwaka 1985, pamoja na concern zilizojitokeza kwa upinzani, hili la kutambua kwamba hawawezi kuleta mabadiliko ya kisiasa hadi tu pale watakapoungana, na vyama vinne vimeungana, kuna sababu bora zaidi ya kusupport mabadilko kwa sasa kuliko wakati mwingine wowote. Propaganda kabla ya uchaguzi zitakuwa nyingi lakini sauti ya mabadiliko ya kisiasa nchini siku zote itakuwa ya juu zaidi. Ni maamuzi yetu ama tubadili mfumo au tuendelee kama tulivyo.

Lowassa amekuwa subject ya mazungumzo na utata. Vinara wa mfumo hodhi wa sasa wanajenga hoja kwamba sasa hivi mabadilko hayawezekani tena kwa sababu ya Lowassa. Nalipinga hili kwa sababu kuu mbili: 1. Mabadilko ambayo nayataka kisiasa hayajajengwa juu ya imani kwa mtu fulani. Yamejengwa juu ya haja kwamba mfumo mpya hautachukulia kila kitu poa, mfumo mpya utakuwa unaelewa kwa nini nimewaweka wao nikawaacha wale. 2. Mungu hutelekeleza azma yake bila kujali wanadamu. Mipango yake haitegemei wanadamu kwa sababu hubadilika. Ibrahimu katika msahafu aliahidiwa na Mungu kupewa mtoto na kwamba uzao wake utakuwa mwingi kama mchanga wa bahari. Baada ya miaka kadha Ibrahim hakupata mtoto kama alivyotegemea. Wakakubaliana na mke wa Sarah amwingie mjakazi, wakapata mtoto. Ibrahimu alikosea lakini bado Mungu alimpa mtoto kutoka katika viuno vyake. Mungu alikuwa anataka kuleta mfumo wa taifa kupitia Ibrahim. Vivyo hivyo nikifikiria Tanzania kuna siku lazima mfumo wa utawala utabadilika si lazima upitie kwa chama fulani unaweza kupitia kwa vyama (kama sasa hivi) au chama kingine, Hata kama kibinadamu kina mawaa. Mawaa si ajabu maana hata mfumo unaotawala sasa hivi una mawaa tena makubwa tu. Ni muhimu basi kuamua ama kuubadili au kubaki kama tulivyo na kuendelea kuwa nchi ya walalamikaji.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

What’s this?

You are currently reading Mabadiliko ni mchakato endelevu, yasipoleta tija kuna n’gwe ya pili, tatu nk at kadulyu.

meta

%d bloggers like this: