Aliyewahi kuwa mpiganaji wa mstituni, Rais maskini kuliko marais wote duniani: Rais wa Uruguay ndugu Mujica aachia madaraka

March 3, 2015 § 1 Comment

Imechapishwa: March 01, 2015 12:36

Imeandikwa mwanzo na Reuters/Andres Stapff

kutafsiriwa na kadulyu.wordpress.com March 2, 2015

Mujica 1

Rais wa Uruguay, Jose Mujica, almaarufu ‘Pepe’, ambaye aliwahi kuwa mpiganaji wa msituni, ambaye muda wote amekuwa akiishi katika shamba lake amekuwa akitoa sehemu ya mshahara wake kwenye shirika la misaada, sasa ameachia madaraka baada ya kutawala miaka mitano, amekamilisha muhula wake akiwa mmoja wa viongozi maarufu sana duniani.

Mujica, (79), anaondoka madarakani akiwa na ukubali wa asilimia 65 ya watu wa Uruguay. Ameheshimu katiba inayomzuia kugombea vipindi vinavyofuatana.

Yeye anasema, ‘Nilipoanza kuwa rais nilijaa nadharia, lakini baadaye ukweli uligonga’, alisika akisema alipohojiwa gazeti la wiki hii la AFP.

Baadhi humwita “Rais maskini kuliko wote duniani”. Wengine, “Rais ambaye kila nchi wengependa wawe naye”. Lakini Mujica husema, “Bado kuna mengi ya kufanya” na ana matumaini kwamba serikali ijayo, itayoongozwa na Ndugu Tabare Vasquez (Ambaye kachaguliwa kwa mara ya pili Novemba mwaka jana) atakuwa, “bora kuliko mimi na atakuwa na mafanikio makubwa

Mujica amefanikiwa kuiweka Uruguay katika ramani ya dunia. Amefanikiwa kuibadili nchi ya wafugaji ya watu milioni 3.4 kuwa nchi inayouza nishati nje, Brazili ikiwa nchi inayoongoza kama soko lao (ikifuatiwa na China, Argentina, Venezuela na Marekani).

Uruguay's President Jose Mujica speaks beside his dog  Manuela during an interview with Reuters in his farm in the outskirts of Montevideo

Uchumi wa Uruguay wa Dola za kimarekani billion 55 umekuwa ukikua kwa asilimia 5.7 kila mwaka kuanzia mwaka 2005, kwa mujibu wa benki ya dunia. Deni la Uruguay likilinganishwa na pato la taifa (yaani uwiano kati ya deni na patoa la taifa – debt-to-GDP ratio) limekuwa likipungua kutoka asilimia 100 mwaka 2003 hadi asilimia 60 mwaka 2014. Kwa muda huo pia gharama za deni hilo zimepungua pia ikiwemo matumizi ya dola kutoka asilimia 80 mwaka 2002 hadi asilimia 50 mwaka 2014. Takwimu hizi bila shaka zinadhirisha taifa linaloongozwa na mtu makini.

Mwenyewe anasema, “Tumekuwa na miaka chanya ya usawa. Miaka kumi iliyopita Waurguay asilimia 39 waliishi chini ya kiwango cha umaskini; tumeshusha kiwango hicho hadi asilimia 11 tu na tumepunguza watu wanaoishi katika umaskini uliokithiri kutoka aslimia 5 hadi 0.5”.

Baada ya kushindwa kwa jitihada za nchi za Amerika ya kusini kwenye vita dhidi ya madawa ya kulevya, nchi hii ya Amerika ya kusini ikawa nchi ya kwanza duniani kuhalalisha matumizi ya bangi, Mujica alisimamia hoja kwamba biashara ya madawa ya kulevya ni hatari zaidi ya bangi yenyewe. Huo ndio ulikuwa msimamo wake sie kwetu hapa bangi ng’o. Japo nasikia kuna watu wametajirika sana na bangi hapa kwetu Tanzania.

Kwa kweli ni miongoni mwa marais wenye upeo mkubwa katika eneo la Amerika ya Kusini. Ingawa Mujica amefanya mambo mengine ambayo hayakubaliki katika jamii na imani zetu kama kuhalalisha ndoa za jinsia moja, amekuwa rais wa kwanza kuwakubali wazuiwa wa Guantanamo Bay kule Cuba. Wazuiwa wa Marekani 6 ambao walikuwa hawajashitakiwa kwa kosa lolote walikaribishwa Uruguay kama wakimbizi. Hawa walikuwa Wasyria wanne, Mpalestina na Mtunisia. Ingawaweje waliruhusiwa kuachiwa tanu mwaka 2009, Marekani haikuwaachia hadi pale rais wa Uruguay alipokubali kuwapokea.

Uruguay's President Jose Mujica waves to the people after receiving the Uruguayan flag on the last working day of his term in Montevideo

(Reuters/Andres Stapff)

Ndani ya mafanikio hayo na utata katika maamuzi hasa ya mambo ya kijamii, tukumbuke kwamba rais Mujica alikuwa kiongozi wa wapiganaji waasi wa msituni wa mrengo wa kushoto, alifungwa miaka 13 jela wakati wa utawala wa kidikteta na kijeshi. Alihimili mateso na miezi mingi ya kuwekwa upweke. Lakini pamoja na yote Mujica anasema hajutii muda wake gerezani bali anaamini ulimsaidia kujenga tabia yake. Wengi leo ugumu tunaulaani japo wakati mwingi hutusaidia kutujenga. Raha maisha yote ya ujana, kula kulala havijengi vinaharibu.

Ukarimu wa Rais Mujica unaongea mengi na makubwa: Alikataa kuhamia Ikulu ya kifahari ya Uruguay ambapo ndio makao rasmi ya Rais, badala yake akachagua kuishi shambani mwake nje ya mji wa Montevideo akiwa na mkewe na mbwa kilema wa miguu mitatu. Pepe kama anavyojulikana alitoa asilimia 90 ya mshahara wake  mfuko wa misaada kwa maskini akisema hakuhitaji mshahara huo. Anaendesha gari aina ya Volkswagen Beetle ya mwaka 1987!

Mujica 4

Mwaka jana, Mujica alikataa ofa ya dola millioni moja kutoka kwa shehe wa kiarabu alotaka kununua gari lake. Pepe alikataa kuuza gari yake hiyo akisema, atawaudhi, ‘Marafiki zake ambao walichangia kuwanunulia hilo gari”

Alivyo mtu wa pekee kuna siku moja aliwahi kusimama na kumpa lifti kijana aitwaye Gerald aliyekuwa amesimama pembeni akiomba lifti. Aliposhushwa alishukura sana na kushangaa kupewa lift na rais wa nchi maana wote walimpita lakini yeye alisimama na kumsaidia.

Mwisho

Kiongozi bora ni yule anayemaindi mabadiliko chanya ya watu na nchi yake na si yule anayeangalia mabadiliko yake tu. Viongozi wengi wameshindwa kuleta mabadiliko katika nchi zetu kwa tamaa tu ya kutajirika utajiri ambao kiuhalisia hatuendi nao popote. Wakati huu watu wanapofikiria kuwa viongozi katika ngazi mbalimbali wajihoji nia hasa yao nini? Ni kusavaivu tu kwa sababu hawana namna nyingine ya kuishi ama wanajitoa kwa ajili ya nchi yao hata kama wao watakufa maskini lakini potelea mbali nchi isonge? Ufisadi ambao tumekuwa tukiushuhudia kwa viongozi wetu kila kukicha unatisha na hauleti matumaini ya ama muda mfupi au mrefu. Ni bahati mbaya sana hakuna mgombea wa urais katika wale waloonyesha nia anayeyaona haya zaidi ya kujenga mfumo wa kulindana. Nani atatoka kama Mujica wa Uruguay?

Advertisements

§ One Response to Aliyewahi kuwa mpiganaji wa mstituni, Rais maskini kuliko marais wote duniani: Rais wa Uruguay ndugu Mujica aachia madaraka

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

What’s this?

You are currently reading Aliyewahi kuwa mpiganaji wa mstituni, Rais maskini kuliko marais wote duniani: Rais wa Uruguay ndugu Mujica aachia madaraka at kadulyu.

meta

%d bloggers like this: