Baadhi ya Maswali muhimu kujiuliza kwa anayetaka kuwa Rais wa Tanzania

September 4, 2014 § Leave a comment

Kuna baadhi ya Watanzania wameanza kutangaza nia ya kuwania cheo cha juu kuliko vyote nchini, Urais wa Tanzania. Ni haki ya kikatiba raia yeyote mwenye akili timamu na aliyetimiza Umri tajwa katika katiba kuomba au kutaka uongozi wa ngazi yoyote ikiwemo Urais. Tena japo kuna sarakasi imechezwa na wenye nacho wanaotaka kuhodhi uongozi wa nchi hii, mtu yeyote ama binafsi au kupitia kikundi cha watu (chama) ana haki ya kuomba kuongoza nchi hii.

Kumekuwa na mijadala kuhusu majina ya watu walioonyesha nia hiyo na baadhi ya watu wanataka sana tujadili masuala na siyo watu. Japo ni vigumu sana kutenganisha masuala na watu maana kama wazee wangu wa kale walivyowahi kusema maneno hayaendi kwa mti bali kwa mtu. Twaweza kuwapima wanaotaka uongozi wa nchi hii kwa nia zao, rekodi zao za maisha na uongozi, na hoja zao juu ya mambo muhimu katika nchi yetu au wengine huita sera, wanasemaje juu ya mambo hayo.

Ili nchi iendelee inahitaji:
– Watu (wenye elimu yenye ustadi),
– Siasa safi (Zinazotoa haki kwa wote kushiriki katika mambo ya nchi),
– Uongozi bora (wenye ufanisi na usio na chembe ya ufisadi),
– Ardhi na maji (yenye rasimali zinazotumika kwa manufaa ya kila mwenye nchi)

Tangu tupate uhuru maadui zetu wakubwa wameendelea kuwa:
– Maradhi (magonjwa yanayokingika na ikishindikana basi yatibike)
– Umaskini (tena uliokithiri)
– Na Ujinga (Elimu inazidi kudorora watu wasiojua kusoma na kuandika wamekuwa wengi kuliko miaka ya 80)

Katika mambo niliyotaja hapo Tanzania haitasonga hadi tumepata viongozi wa kuyashughulikia hayo mambo kwa dhati ili kuleta ukombozi wa pili wa nchi yetu.

Baadhi ya maswali ambayo wenzetu wanaotaka Urais inabidi watujibu kwa dhati kabisa kwa leo ninayo haya matatu:

Unataka kuwa Rais ajaye wa Tanzania, ‘Ni nini hasa kinakusukuma?’

Unataka kuwa Rais ajaye wa Tanzania, ‘Uchumi wetu unakua kwa wastani wa 7% lakini bado kuna ufukara wa kutisha miongoni mwa walio wengi, kitu gani kinaenda vibaya? Utakirekebishaje?

Unataka kuwa Rais wa Tanzania ajaye, ‘Mchakato wa katiba umeenda ndivyo sivyo na unaelekea kwa mara ya kwanza kuwagawa Watanzania, utafanya nini kuleta umoja tuliojivunia tangu uhuru?

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

What’s this?

You are currently reading Baadhi ya Maswali muhimu kujiuliza kwa anayetaka kuwa Rais wa Tanzania at kadulyu.

meta

%d bloggers like this: