Hivi Tanzania tuna demokrasia ya vyama au ya chama?

July 20, 2014 § Leave a comment

Kwa munda mrefu sasa Watanzania tumeshuhudia migogoro ndani ya vyama vikuu vya upinzani ukianzia NCCR ya wakati ule, CUF na sasa CHADEMA nadhani ndio miongoni mwa vile vinavyounda UKAWA kwa sasa. Inavunja moyo sana Watanzania wenye hamu ya mabadiliko ambayo wengi wamedhani yatakuja kupitia chama kingine chochote na si CCM. Migogoro mingi imekuwa juu ya madaraka ndani ya vyama hivyo. Haianzii kwa wananchi, inaanzia kwao viongozi na hatimaye kwenye vikao vyao ambavyo sisi wananchi hatuhusiki. Mara vyombo vya habari huchukua hizi agenda za ugomvi wa viongozi na kuzileta kwa wananchi. Ambao nao huishia kuwa na mirengo yao, aghalabu huchagua upande katika pande mbili zinazoshindana na huo ama huwa mwisho wa umaarufu wa chama husika ama huzorota.

Twapaswa kuchukua tahadhali kujiingiza katika siasa za ugomvi wa ndani ya vyama. Mimi nasukumwa zaidi na kuangalia picha kubwa. Ni namna gani tunaweza kuleta mabadiliko katika nchi hii? Je ni kweli walio wengi wanataka mabadiliko au ni wachache tu ambao mara nyingi wanaitwa wasomi? Je mabadiliko haya ni ya muhimu, na kama ni ya muhimu kwa nchi yetu ni namna gani tutawasaidia wengine waelewe umuhimu huu wa mabaliko? Je, tusubiri chama fulani kiiondoe CCM ndio tuanze mabadiliko? Au wananchi tusukume mabadiliko tuyatakayo kila mmoja katika eneo lake la mvuto?

Wengi tunaamini katika demokrasia tatizo hasa ni demokrasia ya namna gani. Wengi tuliona Libya haina demokarasia hilo halina ubishi. Ubishi wetu na nchi za magharibi ambazo ndizo zinadhani ni miamba ya demokrasia, ni jinsi ya kuleta demokrasia Libya, Iraq, Syria na kadhalika. Kuchukua nafasi ya CCM kunaweza bado kusitibu matatizo ya demokrasia ya Tanzania, ingawaje itakuwa dalili nzuri kwamba wananchi wanaweza kuamua jambo likatendeka. Hiyo ni dalili njema.

Tanzania tuna demokrasia ya vyama vingi hilo halina ubishi pia. Baadhi tunaona kwa sababu ya CCM kuendelea kutawala hatuna demokrasia kamili. Wengi pia hatuelewi kwamba Tanzania hatuna demokrasia ya vyama vingi tuna demokrasia ya CCM iliyoruhusu kuwepo kwa vyama na inayotoa imla ya namna gani ipingwe (it dictates how it should be opposed). Wanasiasa walioko upinzani ama wanalielewa hili au kwa kukinzwa na maslahi binafsi hawalioni. Katika vita yoyote ni muhimu kumfahamu adui yako: Ni nani, anauwezo gani, yuko wapi. Inawezekana kabisa adui wa vyama vya upinzani si CCM kama wengi wanavyodhani na ndiyo maana vinaenda hatua tano mbele halafu vinarudi hatua kumi nyuma. Chama tawala wanaliona hilo na ndio maana wanasema CCM itaendelea kutawala milele. Si kweli lakini bila upinzania kujua nani hasa wanampinga itachukua muda kwenda ikulu kama wenyewe wanavyoita.

Viugomvi ndani ya vyama vya hapa na pale ni wahusika kupoteza picha kubwa na kukosa kuunganisha na mawazo ya umma na tamanio lake. Wanajiona wenyewe hawaioni nchi na shida yake. Nashauri Upinzani wote wadogo na wakubwa wajiulize wanampinga nani hasa.

Kwa swala la Chadema, si kweli kwamba kumwondoa Dr. Slaa na Mbowe katika uongozi wa chama na kumweka Ndugu yangu mwingine yeyote, kutaimarisha demokrasia ndani ya Chadema na hatimaye kuwa mfano bora na kujenga imani kwa wananchi na wapiga kura. Kwamba kuwatoa Dr Slaa na Mbowe kutatoa picha kwa wapiga kura kwamba Chadema inaheshimu demokrasia na hivyo inafaa na kuaminika kupewa kuongoza nchi. Si rahisi kiasi hicho!

Ni kweli kiongozi yeyote anatakiwa kuheshimu taratibu walizojiwekea lakini si sahihi kudhani kwamba tatizo la chama husika ni Mbowe, Slaa na zitto tu basi. Tatizo si yeyote miongoni mwao, tatizo ni TATIZO, lakini tatizo kubwa huenda miongoni mwao haliwajui tatizo.

Mfano mdogo tu, mwaka 2010 zaidi ya nusu ya wale waliojiandikisha hawakupiga kura. Viongozi wa vyama wanapaswa kuelewa tatizo la nchi yetu. Wakifanya hivyo watajua adui halisi si wao kwa wao. Kuunda vyama zaidi hakutaongeza wapiga kura wala demokrasia, sana sana kutawagawa tena watakopungua zaidi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

What’s this?

You are currently reading Hivi Tanzania tuna demokrasia ya vyama au ya chama? at kadulyu.

meta

%d bloggers like this: