Matatizo ya Watanzania ni Makubwa Kuliko Vipimo vya GNP na GDP

January 26, 2014 § 1 Comment

Watu wa zamani kama kina Newton, Galileo, Faraday, na wa mwisho mwisho kama kina Einstein walikuwa wanafikiri sana. Na kufikiri kwao kumeleta mapinduzi katika jamii.

Wapo pia Watu wa zamani kama kina Newton, Galileo, Faraday, na wa mwisho mwisho kama kina Einstein walikuwa wanafikiri sana. Na kufikiri kwao kumeleta mapinduzi katika jamii.

Wapo pia waliofanya hivyo katika Nyanja za uchumi na jamii. Leo tunatumia nadharia zao bila kufikiri wala kuhoji zaidi ili ikiwezekana tugundue au kuboresha nadharia zao ili zifae kutumika katika kizazi hiki. GNP, GDP n.k vililalia kwenye urahisi. Maisha ya watu huwezi kuyapima kwa rula. Mwanadamu ni mchanganyiko (complex) huwezi kuweka vipimo rahisi hivi kusema yuko na hali gani kijamii. Mfano Tanzania inasemwa kwa sasa hivi uchumi wake unakua kwa haraka na baadhi ya wanasiasa na watawala wanafurahi na kujitapa, lakini hali ya wananchi ikoje?

Uchumi mzuri si tarakimu tu bali ubora wa maisha kwa watu. Leo baada ya miaka 50 ya uhuru bado tunataabika na maji, huduma dhaifu za afya, elimu inayodorora kila kukicha, huduma ya nishati isiyo na uhakika, makazi hafifu, miundo mbinu isyokidhi mahitaji ya watu, matatizo lukuki ya kiuongozi na utawala bora na kadhalika. Kujitapa kwa kipimo kimoja tu ni sawa na kutupa punje moja ya mchanga baharini ukitegemea upate wimbi la kuitikisa meli ya mizgo.

Vipimo vingine vinavyohusiana na ubora wa maisha ya mwananchi hatuvijali, tunajali na kuheshimu vipimo vya wakubwa wanaoutupa hela. Juzi mmoja wao kaandika makala ya kutudharau, wafuatiliaji wa mambo mtakuwa mmesoma makala ya tajiri aliyepindukia ndugu William Gates (almaarufu Bill Gates). Anasema tatizo la dola chache zinazopotea katika rushwa ya misaada wanayotupa si kitu ukilinganisha na faida ya misaada hiyo kwetu! Ni dharau kubwa kwetu watanzania. Sikumbuki tarakimu kwa haraka lakini sote tunajua ufisadi unavyokula sehemu ya bajeti yetu kila mwaka. Maisha yanayopotea kwa ajili rushwa. Hivi kweli mama na mtoto wanaofariki kwa kukosa kutoa kitu kidogo ama kwa daktari au kwa nesi thamani yake Bill Gates anaijua? Ufisadi katika nyanja muhimu za uchumi ambazo zingetuletea mabadiliko na badala yake wanafaidika wajanja wachache na wageni anaufahamu?

Inakera sana! Nawasihi watanzania wote kila mmoja katika sehemu amabayo ana mvuto fulani (individual sphere of influence) afanye kitu tuokoe hii nchi. Si mambo ya mzaha haya ni mambo nyeti.

J2 njema

Advertisements

§ One Response to Matatizo ya Watanzania ni Makubwa Kuliko Vipimo vya GNP na GDP

  • Stephen Jaoko says:

    Kwakweli nimeguswa na hili andirons watanzania tulip Wendi tumekua tukidangaywa kila siku majukwaani na wanasiasa wakijaribu kutueleza jinsi ambavyo uchumi wa nchi yetu unavyokua kwa kasi wakati huo humdrum a muhimu Kama vile elimu na Anya zikizidi kuzorota kwa kasi,sasa sijafahamu wale wanaozifanya hizi research wanatumia vigezo vipi kupata hizo data Watanzania we really need every one to play his part so that we can take this country some where

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

What’s this?

You are currently reading Matatizo ya Watanzania ni Makubwa Kuliko Vipimo vya GNP na GDP at kadulyu.

meta

%d bloggers like this: