Tuuangalie muungano wa Tanganyika na Zanzibar Kimahesabu

August 15, 2013 § Leave a comment

Tuna njia nne za kuutegemeza muungano wetu hebu tuzitafakari na kuzichambua ipi ingetufaa. Bwana Asenga Abubakar aliandika hivi (kwenye facebook yake):

1+1= Tanganyika+ zanzibar =3

Mbona mwalimu wangu wa hesabu Nyerere alinifundisha kuwa 1+1=2

Inamaana akuwa sawa?

Nisaidieni 1+1 ni ngapi?

CCM itampakata mtu 2015 na ata acha siasa moja kwa moja

Nikamjibu ifuatavyo:

Asenga Abubakar Kwa hesabu zako hizo hili somo litaendelea kuwa mgogoro nchini. Nani alikwambia kwamba thamani ya Zanzibar ni moja na thamani ya Tanganyika ni moja? Na hiyo 2 inanakuwaje inageuka kuwa serikali kama ulizojumlisha ni nchi? Ulimwengu gani wa hesabu unajumlisha vitu vya aina moja halafu jumla inakuwa vitu vingine i.e unajumlisha mbuzi halafu jibu linakuja nge? Japo idadi itakuwa 2 lakini hao si mbuzi tena. Muungano wa nchi uanaathiri baadhi ya variables lakini kijiografia hizi nchi zinaendelea kuwepo.

Kulazimisha model ya kimahesabu kuelezea muungano na kwa nini tuna serikali mbili badala ya 1 au 3 si sahihi. Hili si jambo la kimahesabu ni jambo la kisiasa. Kama nchi inawakilishwa na serikali basi mlinganyo ulioutoa si sahihi pia. Kama 1 ni serikali ya Zanzibar na moja nyingine ni serikali ya Tanganyika, kulia mwa mlinganyo wako unatakiwa upate selikali ya Zanzibar na serikali ya Tanganyika, lakini zilizopunguzwa madaraka yatakoyopewa serikali ya Muungano, ndiyo mlinganyo wako utakuwa sawa.

Ili muungano uheshimu sheria ya kujumlisha inabidi uwe hivi:

Serikali ya Tanganyika + serikali ya Zanzibar = serikali ya Tanganyika iliyopunguzwa madaraka + serikali ya Zanzibar iliyopunguzwa madaraka + serikali ya Jamhuri ya Muungano inayochukua madaraka yaliyopunguzwa kwenye serikali ya Tanganyika na Zanzibar. Kimahesabu unaweza kupunguza madaraka ya nchi zote mbili ukayaweka yote kwenye muungano. Kupunguza madaraka ya nchi moja kuwa sifuri halafu nyingine wanabakisha madaraka yao fulani ni muundo tepetevu. Mfumo huu unaifanya nchi moja kujiona ndio imeungana zaidi kuliko ile nyingine. Na ile nyingine itaendelea kutamani kuwa autonomous kwa sababu ya utamu wa madaraka inoyoyaonja kila siku. Kwa mfumo huu Tanganyika ndio imeungana zaidi kuliko Zanzibar. In logic we say fallacy!

Kisiasa je muungano tunautaka? Kama tunautaka wa namna gani?

Hebu bofya hapa chini uangalie hesabu za muungano wetu:

Muundo wa Muungano Kimahesabu

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

What’s this?

You are currently reading Tuuangalie muungano wa Tanganyika na Zanzibar Kimahesabu at kadulyu.

meta

%d bloggers like this: