Tamko la Waziri Mkuu kuamuru wahalifu kupigwa na polisi: Una maoni gani?

June 21, 2013 § 1 Comment

”Ukifanya fujo, umeambiwa usifanye hiki ukaamua wewe kukaidi UTAPIGWA TU! Eh, Maana HAKUNA NAMNA NYINGINE eh, maana lazima wote tukubaliane kwamba nchi hii TUNAIENDESHA KWA MISINGI YA KISHERIA. sasa kama wewe umekaidi hutaki unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndio jeuri zaidi WATAKUPIGA TU, NA MIMI NASEMA/naagiza MUWAPIGE TU, KWA SABABU HAKUNA NAMNA NYINGINE, eh, MAANA TUMECHOKA SASA!”

Nimesikiliza maneno ya Mheshimiwa Waziri Mkuu nikashangazwa sana. Sababu zilizonishangaza ni hizi zifuatazo.

1. Ni tamko linalokuja baada ya matukio ya Arusha na Mtwara. Ambako kote imeonekana Jeshi letu limekuwa brutal kwa raia wasio na hatia.

2. Tamko linanakuja baada ya kuonyesha kwamba polisi wamekuwa wakitumika sana kuingilia shughuli za vyama vya siasa ikiwemo mikutano na maandamano ya amani hasa ambavyo vimekuwa vikifanywa na Chadema.

3. Polisi hutumia nguvu za ziada kumthibiti mhalifu ili wamfikishe kwenye vyombo vya sheria na sio kumwadhibu wao wenyewe. Polisi hawawezi kufanya kazi ya kukamata na kuhukumu na kutoa adhabu. Waziri anasema, kwa kweli anaagiza wahalifu wapigwe tu.

4. Polisi wamekuwa wakitumia sheria za kudhibiti mikusanyiko vibaya na ni uvunjaji mkubwa wa haki za msingi za binadamu. Yaani haki kukusanyika, kujumuika na kutoa maoni. Sheria hizi ni kikoloni. Zilitumika kudhibiti harakati za ukombozi kutoka kwenye makucha ya ukoloni. Ni sheria ya kipuuzi sana kutumika kwenye nchi ya watu walio huru.

5. Mikusanyiko ambayo imekuwa ikilengwa ni hasa ya kisiasa au ya kiharakati. Mikusanyiko mingine kama ya arusi, mazishi, makanisani na misikitini n.k haina tatizo. Wananchi wanakusanyika bila kuomba kibali wala kupatiwa ulinzi wa polisi, labda tu kama kuna kiongozi mwandamizi anakuja kwenye hiyo mikusanyiko. Lakini mikusanyiko ambayo wananchi wanataka kukutana kujadili hatima zao kisiasa inautumiwa sheria ya mikusanyiko isiyo halali kuidhibiti. Hii si haki hata kidogo.

6. Tamko la Waziri Mkuu ni Tamko la Serikali. Kwa namna ambavyo Jeshi letu limekuwa likitenda, yaani tayari linavunja katiba na haki za binadamu, hali itakuwaje askari wanapoona kwamba matendo yao ukatili yanabarikiwa na Waziri Mkuu?

7. Tamko hili linatoa mibaraka kwa askari kutenda uovu kwa wananchi, kutumia silaha walizopewa kulinda maisha na mali za wananchi vibaya huku wakijua ni mambo ambayo serikali imeruhusu.

8. Ndio maana Serikali haichukui hatua madhubuti kuadhibu askari wanaotuhumiwa kufanya mauaji na ukatili kwa wananchi. Raia tunaona tunaelekea kwenye udikteta zaidi.

9. Kuna msemo umezoeleka sana kwamba Jeshi la Polisi litamchukulia mtu fulani ‘Hatua kali za kisheria’. Maana yake hasa nini kwa nchi inayofuata mfumo wa kidemokrasia na utawala bora? Jeshi halina hatua kali za kisheria zaidi ya kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha mahakamani. Hizo ni hatua za kawaida na siyo ‘kali’ kama polisi wanavyotishia watu. Ukali wa sheria ni pale utakabainika pasipo shaka yoyote kwamba mtu ametenda kosa. Neno hili ‘Hatua kali’ limekuwa likitumika kumaanisha mateso ambayo polisi humfanyia mtuhumiwa hata kabla ya kumpeleka mahakamani na ndiyo maana wananchi huogopa polisi zaidi badala ya kuogopa madhara ya kuvunja sheria.

10. Tamko hili linaweza kutafsiriwa kama baraka ya kumpa mtu adhabu kinyume cha sheria au kujichukulia sheria mikononi dhidi ya watuhumiwa (extra judicial punishment).

Tusaidie kuokoa nchi yetu isiangamie kwa kutunza amani, kuheshimu haki za binadamu na kuzilinda. Wandamanaji au mikusanyiko isiyokuwa na vurugu haivunji sheria yoyote hata kama ikifanyika bila ruksa ya polisi. Hatuwezi kuitoa sadaka haki ya kukutana tutakavyo mikononi mwa watu wengine.

Advertisements

§ One Response to Tamko la Waziri Mkuu kuamuru wahalifu kupigwa na polisi: Una maoni gani?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

What’s this?

You are currently reading Tamko la Waziri Mkuu kuamuru wahalifu kupigwa na polisi: Una maoni gani? at kadulyu.

meta

%d bloggers like this: