Tanzania ina Gesi nyingi, Je mikoa itokayo hiyo mali asili, waachiwe asilimia ngapi ya mapato?

May 29, 2013 § Leave a comment

Maoni haya ni kutokana na habari iliyochapishwa kwenye Gazeti la Mwananchi Mei 29, lenye kichwa cha habari, ‘Jeshi lafanikiwa Kudhibiti vurugu Mtwara’

Issue ya Mtwara ni uwakilishi wa jinsi wananchi waTanzania wasivyorika na uvunaji wa maliasili zetu Tanzania. Kuna vitisho sasa vinatolewa kwa wananchi wanaotaka utengemavu wa namna tunavyoshiriki katika keki hii ya Taifa. Kwanza tu nikanushe vitisho vya vita vya wenyewe kwa wenyewe eti kwa sababu ya gesi ni madai ya kipuuzi. Kwa nini? Mpaka sasa kinachotekea ni vita kati ya majeshi ya serikali na wananchi. Ni kitu kisichofikirika eti Wachaga ama Wasukuma watachukua mikuki na mapanga eti wakawapige wamakonde kwa kuzuia ujenzi wa bomba la gesi kuja Dar. Hata vitisho vya vita vya kidini vinafanya na wanasiasa wetu uchwara kama propaganda ya kuhalisha kukosa sera kwao.

Ni ukweli ulio dhahiri kwamba watanzania haturidhiki na jinsi ambavyo mali asili inavunwa na kuishia kwa mikono ya wachache na wawekezaji. Tumeambiwa kwamba mali asili ni ya nchi nzima. Kwani hasa nchi nini? Hivi ni wapi Mtwara utakuta kitu cha kusema kwamba wamefaidika na dhahabu na almasi vinavyochimbwa Geita na Mwadui? Mwadui pale zamani walau kulikuwa na shule nzuri tu ya sekondari, hospital na uwanja wa ndege (enzi za Mwalimu), sasa hivi viko wapi? Tunaachiwa mashimo tu pale. Walau tutabaki na nyumba! Geita Gold Mine hamna kitakachobaki zaidi ya mashimo na sumu ya Cyanide. Nyumba zenyewe za makaratasi! Faida tunayopata nchi ni ndogo sana ukilinganisha na mali inayochumwa pale. Tuliingia mikataba kama vipofu. Wahusika watajalipa siku moja.

Mji wa Geita shida tupu, hata maji ya shida. Kama dhahabu haijasaidia hata watu waishio pale iweje uzungumzie eti dhahabu ni mali ya nchi nzima. Nchi ni nani? Je, ni mawaziri wachache wanaosaini mikataba ambayo ni siri kati yao na wawekezaji ndiyo nchi? Hivi tunamwaminije Waziri wa Nishati kusaini mikataba (hata kama amesaidiwa na mwanasheria mkuu), kwa nini isiwekwe wazi? Mbona haya makampuni hesabu zake ziko wazi ulaya halafu kwetu eti ni siri?

Halafu kuna watu wanalinganisha gesi, dhahabu na almasi na viazi, mahindi na pamba. Hili ni tatizo tu la elimu yetu. Inakuwaje mtu anashindwa kuelewa kwamba mazao ya kilimo yanaendeshwa kufuata mfumo wa biashara linganifu. yaani willing buyer and willing sellers. Mazao ya kilimo ni miliki ya mtu binafsi si mali asili.

Waziri wa Nishati na Madini anaharakisha kusaini mikataba ya kuchimba gesi na mafuta bila sera ya nchi kuwa tayari kwanza. Sera ndiyo itatoa dira mali ivunweje na mapato yagawiweje. Mfano Kenya wamegundua mafuta kule Turkana, na tayari wananchi wa hiyo county wanadai asilmia 25 ya mapato ibaki maeneo ya pale mafuta yalipo, Serikali wamepanga ibaki asilimia 15. Kwa habari zaidi soma: http://www.ratio-magazine.com/201206154114/Kenya/Kenya-Turkana-Oil-Revenues-Great-Expectations-First-Trouble.html
Sisi tunazungumzia kule Kilwa asilimia 0.3! yaani hata asilimia 1 haifiki na ndicho kinachoahidiwa Mtwara pia. Halafu wananchi wa Mtwara wakitoa hoja tunawatwanga. Kwa nini asilimia 0.3 imeandikwa kwenye jiwe?

Ripoti ya leo kwenye gazeti la The citizen imesema kuna Dollar bilioni 5.9 za kimarekani wanzetu yaani watanzania wenzetu wameficha nchi za nje. Hizi ni sawa na shilingi Trillion 9.44, budget yetu ya mwaka jana kama sikosei ilikuwa Trillion 15. Si ajabu ukakuta wenye fedha hizi wengi wao ni hawa hawa tuliowapa dhamana ya uongozi au wenye mahusiano ya karibu na viongozi au wapambe wao. Halafu leo mtu aseme mali asili ni kwa ajili ya nchi nzima? Kama ingekuwa imedhihirishwa hivyo kwenye dhahabu na almasi watu wa Mtwara wangeona mfano na wala wasingekuwa na matatizo, lakini ni kinyume! Umaskini wa kutupwa ndio umewakalia watu wa Mwanza, Shiyanga, Tabora, Kagera na Mara.

Ninamsihi Waziri husika na serikali tutengeneze kwanza sera ya mafuta na gesi halafu ndio tuendelee na kuchuma hii mali asili. Sera itaonyesha wazi mgawano wa mapato utakuwaje na hatima ya nchi kwenye mikataba hii itakuwaje.

Mawasiliano
Serikali iwe na mfumo mzuri wa mawasiliano na wananchi. Kwanza tunapenda kuwe na uwazi katika mikataba hii ya uvunaji wa mali asili. Ili tuwe na uhakika kwamba sera ya msingi na sheria husika zimefuatwa na wahausika. Kutumia Press Realease (Taarifa kwa vyombo vya habari) si sahihi. Kwanza haiwafikii walengwa labda tu kama walengwa ni hawa tuaosema nchi za magharibi. Kama ni wananchi wa Tanzania si mfumo sahihi. Ni muhimu kufanya mazungumzo. Tusiwatishe wananchi ili wafunguke. Hiyo tu itatosha kuanza kuleta suluhu. Isionekane kwamba kuwa nyuma ya msimamo huu walio nao watu wa Mtwara si dhambi. Ni wazo tu lakini tunavyolishughulikia linakuwa tatizo kubwa, hata mmoja amesikika akisema ni uhaini. Tunapofanya hivyo linakuwa ni vuguvugu lisilokuwa na kiongozi, huwezi ku-negotiate na raia wote, unaweza kufanya hivyo na jumuia au taasisi wanazoziheshimu. Hata kama ni chama cha kisiasa kama ndicho wananchi wameona kinabeba wazo lao kisikilizwe. Tuache kutisha raia wanyonge. Wengi wanadhani kuvitisha vyama vya siasa na vya kiraia vikae mbali na vuguvugu hili ndiyo salama. Ni mkakati mbovu. Hata kwenye vita ni heri ujue adui ni nani kuliko kupigana na kila mtu anayepita njiani kwako. Itatugharimu sana kurudisha heshima ya jeshi letu la polisi kule kusini. JWTZ si kazi yao kufanya hivyo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

What’s this?

You are currently reading Tanzania ina Gesi nyingi, Je mikoa itokayo hiyo mali asili, waachiwe asilimia ngapi ya mapato? at kadulyu.

meta

%d bloggers like this: