Mchanganuo wa maoni kuhusu hoja ya udini aliyoitoa Mh. Zitto kwenye FB yake

April 8, 2013 § 4 Comments

Ndugu msomaji utakubaliana na mimi kwamba swala la udini ni tatizo hapa Tanzania kwa sasa na kwamba kila raia, mimi, wewe na yule sote ni sehemu ya tatizo na utatuzi pia. Tabia ya kulaumu wengine na kuwasukumia jukumu la kutatua watu wengine tutazidi kuingia kwenye mgogoro zaidi. Tayari kuna ushahidi kuwa utungwaji wa katiba una misukumo ya kidini tayari na uchaguzi ujao hautaepuka misingi ya kidini kama kila mmoja hatachukua hatua ya kusema hapana.

Leo Mheshimiwa zito ameto hoja kwenye Twitter na FB kama ifuatavyo:

‘Watanzania tunapenda sana kuficha uchafu chini ya kapeti. Chuki za kidini mitaani is real. SMS za chuki zinasambaa. Kuzisema au kuziweka hapa sio kuzitangaza bali Ni kuonyesha Kwa Kiwango gani uvundo wa udini umejaa nchini. Kila namba inayotuma ujumbe wa chuki za kidini ninau report #TCRA lakini SMS hizo zinaendelea. Waislam wanaambiana misikitini kuchaguana kwenye mabaraza ya #Katiba. Wakristo wanaambiana makanisani kuchaguana kwenye mabaraza ya Katiba. Hapo tuna Taifa kweli? Tusifiche mambo haya, tuyaseme waziwazi na kuyakemea Kwa vitendo. Wahenga walisema mficha ugonjwa?…..’ https://www.facebook.com/zittokabwe/posts/562703327083702

Nimeguswa na namna watu walivyotoa maoni yao. Nimeona kwa kutafakari kwangu watu waliochangia hoja hiyo mawazo yao yamegawanyika sehemu kuu tatu na nimeamua kuyachambua kulingana na aina tatu kuu za mawazo hayo:

1. Asilimia 60 kwa namna fulani wamesema, ‘wanaodhani tatizo la udini si langu ni la mtu mwingine’

2. Asilimia 25 kwa namna fulani wamesema, ‘Wanaodhani wanahusika na tatizo na ni sehemu ya utatuzi’

3. Na asilimia 15 kwa maana ya moja kwa moja wana mawazo bila utatuzi wowote

Bofya hapa chini au soma moja kwa moja chati hii kufuatilia uchanganuzi huo. Ni juu yako kuamua kama, Je tukiendelea na fikra za namna hii tutatatua kweli tatizo la udini hapa Tanzania.

Udini Tanzania – Mchanganuo wa maoni yaliyopokelewa kwenye zitto FB

kwa aslimia

Je una mawazo gani juu ya maoni haya? Kazi ni Kwangu, kwako na kwa yule.

Advertisements

§ 4 Responses to Mchanganuo wa maoni kuhusu hoja ya udini aliyoitoa Mh. Zitto kwenye FB yake

 • Mwasumbi sekela says:

  Watanzania tunatatizo la ufinyu wa fikra, ubinafsi pamoja na kutokubali makosa na kutafuta suluhisho.

 • Zainab abdallah says:

  MY OWN POEM..Struugling for change…
  God knows the values of the world, hence we were created, since we r ol part of it, we need to be accepted..
  Lets not put difference, because of religion, it’s such a coincidence, we were born in that region..
  No 1 has ever seen him, or came back from heaven, hating others because of him, you are really mistaken!
  We might have different cultures, but we are not different, since we all aim for success, and we all wish for the future..
  We might have similar ways, or different in earnings, we might have similar days, or different in thinking..
  We might differ in coloursm ideas or facts, we might differ in matters, on being firt and last..
  But as long we all have ears, and we can observe with our eyes, as long we all produce tears, is a fact of being wise..
  Nevertheless how stronger you are, nevertheless what support you might have, the reality of this world, is built by love..
  Life is not all about who you are, life is not all about where you stay, you might own houses and cars, and some they’ll fade away..
  We need leaders who knows what it takes for others to survive, we need leaders who knows what it takes for others to be alive..
  Each and everyone has a part, to play like a hero, together we can work, and build our tomorrow..
  It’s worthless being human, if you can’t prove your humanity, it’s worthless to sound like a man, with no characters and identity..
  May God bless Tanzania and every place else and may God bless Tanzanians and everyone else..
  We need PEACE not PIECES..

 • Tryphon Aloys Kanunshu says:

  NItaanza kwa adithi moja. Siku 1 familia fulani ya mume na mke ilikuwa inasumbuliwa na panya nyumbani kwao, hivyo wakaamua kuchukua hatua kali dhidi ya panya hao na mambo yalikuwa kama ifuatavyo:
  Mume: mke wa ngu mimi naona tununue mtego wa panya
  Mke: Sawa baba nadhani itasaidia kuwapunguza kama si kuwamaliza kabisa.
  Mtego ukanunuliwa, Panya alipouona mtego ule akakimbia nakwenda kwenye banda la KUKU kuomba msaada, Panya alikawaambia kuku; wenye nyumba wamenunua mtego wa panya naomba uende unisaidie kuutoa; kuku wakajibu, mtego wa panya sisi Hautuhusu nenda kautoe mwenye.
  Panya akakimbilia kwenye zizi la mbuzi kuomba msaada vilevile na majibu yalikuwa yaleyale aliyopata kwa kuku.

  Hakukata tamaa akaenda kwenye zizi la ng’ombe pia majibu yakawa n yaleyale. Panya aliamua kurudi ndani.

  Usiku mama wakati anaenda aja akakuta pale alipoweka mtego wa panya kuna kitu kinarukaruka na mtego ule, hivyo akaenda kushuhudia kumbe alikuwa nyoka ambaye aliwekamwatwa mkia, kitendo cha mama yule kusogea karibu nyoka yule aliweza kumng’ata mama yule ni kumwachia sumu kali.

  Mama yule alikimbizwa hospitali, kesho yake mume wake akamwandalia chakula kadri alivyokuwa anampenda mkewe akaamua kuchukua KUKU mmoja kumchinja kwa ajili ya kitoweo cha mgonjwa.

  Baada ya wiki mgonjwa akaruhusiwa kurudi nyumbani, hivyo ndugu wa mke huyo wakaja nyumban kumwangalia, kutokana na ugeni huo mume akaamua kwenda kwenye zizi la mbuzi nakuchukua mbuzi mmoja na kumchinja kwa ajili ya kitoweo cha wageni.

  Bahati mbaya ndani wiki moja baada ya kurudi nyumbani kwa mgonjwa hali ikawa mbaya ya zaidi jambo ambalo lili7bisha kifo chake kutokana na sumu ya Nyoka.

  Sasa kwenye msiba wa marehemu kutokana na wingi wa watu baba mwenye nyumba (mume wa marehemu) aliamua kumchinja ng’ombe kwa ajili ya kitowelo.

  Mwisho Panya aliendelea kuishi kama kawaida.

  Hivyo waTanzania wenzangu tusiwe kama MBUZI na NG’OMBE katika suala hili la UDINI Tuungane kwa pamoja kukemea na kuutokomeza kabisa la sivyo ziiumiazo ni nyasi.

 • OMARY MAKINA says:

  CHUKI ZA KIDINI CHANZO CHAKE NIONAVYO MIMI NI VIONGOZI WA DINI KUKUBALI KUTUMIWA NA WANASIASA. KATIBA YETU IWEKE WAZI MIPAKA YA WANASIASA KUHUSU MASWALA YA KIDINI. VIONGOZI WAKISIASA WAACHE KUWA WAGENI RASMI KWENYE MASWALA YA KIDINI. HILI ZAO LILIPANDWA NYAKATI ZA KAMPENI ZA CHAGUZI ZA RAIS MARA BAADA YA TANZANIA KURUHUSU MFUMO WA VYAMA VINGI.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

What’s this?

You are currently reading Mchanganuo wa maoni kuhusu hoja ya udini aliyoitoa Mh. Zitto kwenye FB yake at kadulyu.

meta

%d bloggers like this: