Mchanganuo wa maoni kuhusu hoja ya udini aliyoitoa Mh. Zitto kwenye FB yake

April 8, 2013 § 4 Comments

Ndugu msomaji utakubaliana na mimi kwamba swala la udini ni tatizo hapa Tanzania kwa sasa na kwamba kila raia, mimi, wewe na yule sote ni sehemu ya tatizo na utatuzi pia. Tabia ya kulaumu wengine na kuwasukumia jukumu la kutatua watu wengine tutazidi kuingia kwenye mgogoro zaidi. Tayari kuna ushahidi kuwa utungwaji wa katiba una misukumo ya kidini tayari na uchaguzi ujao hautaepuka misingi ya kidini kama kila mmoja hatachukua hatua ya kusema hapana.

Leo Mheshimiwa zito ameto hoja kwenye Twitter na FB kama ifuatavyo:

‘Watanzania tunapenda sana kuficha uchafu chini ya kapeti. Chuki za kidini mitaani is real. SMS za chuki zinasambaa. Kuzisema au kuziweka hapa sio kuzitangaza bali Ni kuonyesha Kwa Kiwango gani uvundo wa udini umejaa nchini. Kila namba inayotuma ujumbe wa chuki za kidini ninau report #TCRA lakini SMS hizo zinaendelea. Waislam wanaambiana misikitini kuchaguana kwenye mabaraza ya #Katiba. Wakristo wanaambiana makanisani kuchaguana kwenye mabaraza ya Katiba. Hapo tuna Taifa kweli? Tusifiche mambo haya, tuyaseme waziwazi na kuyakemea Kwa vitendo. Wahenga walisema mficha ugonjwa?…..’ https://www.facebook.com/zittokabwe/posts/562703327083702

Nimeguswa na namna watu walivyotoa maoni yao. Nimeona kwa kutafakari kwangu watu waliochangia hoja hiyo mawazo yao yamegawanyika sehemu kuu tatu na nimeamua kuyachambua kulingana na aina tatu kuu za mawazo hayo:

1. Asilimia 60 kwa namna fulani wamesema, ‘wanaodhani tatizo la udini si langu ni la mtu mwingine’

2. Asilimia 25 kwa namna fulani wamesema, ‘Wanaodhani wanahusika na tatizo na ni sehemu ya utatuzi’

3. Na asilimia 15 kwa maana ya moja kwa moja wana mawazo bila utatuzi wowote

Bofya hapa chini au soma moja kwa moja chati hii kufuatilia uchanganuzi huo. Ni juu yako kuamua kama, Je tukiendelea na fikra za namna hii tutatatua kweli tatizo la udini hapa Tanzania.

Udini Tanzania – Mchanganuo wa maoni yaliyopokelewa kwenye zitto FB

kwa aslimia

Je una mawazo gani juu ya maoni haya? Kazi ni Kwangu, kwako na kwa yule.

Where Am I?

You are currently viewing the archives for April, 2013 at kadulyu.