Je, viongozi wa serikali wanaweza kupewa maelekezo na kiongozi wa dini fulani kuua waumini wa dini nyingine? #ChangeTanzania

February 22, 2013 § Leave a comment

Kuna mjadala unaoendelea kuhusu misuguano ya kidini na hasa imeanzia wapi unaoendelea kwenye blog ya #ChangeTanzania.

Ndugu Aballah aliandika kwamba kuna padri mmoja kwa jina la Padri Camilius aliwahi kutoa amri ya kuua waislam na serikali imekubali kutekeleza amri hiyo. Anasema hayo yameandikwa katika kitabu Kilichoandikwa na Prof Hamza Njozi na anadhani ni ushahidi wa kweli. Kwanza mimi nilikuwa-shocked na habari hizi kwamba kiongozi wa dini fulani anaweza kuipa Amri serikali ikatekeleza tena ya kuua waumini wa dini nyingine. Haya ni baadhi ya maoni yangu kama una Muda yapitie. Tamaa yangu ni kuona Watanzania bila kujali tofauti zetu tunaishi kwa amani, letu likiwa moja tu kuwadai viongozi wetu wa serikali watumie kodi zetu vizuri kusukuma maendeleo lakini sisi pia tukichukua nafasi kila mmoja kwa juhudi zake kuushinda umaskini. Endelea….

Ndugu Abdallah,

Inaonekana huyo Padri Camillius Lwambano wa Kanisa Katoliki ni mtu powerful sana na wa kuogopa. Yaani anaweza kwenda ikulu akatoa amri kwamba waislamu wauawe na rais tuliyemchagua akatii amri ya Padri. Kama  maneno haya ni kweli basi nchi hii ni janga.

Nasukumwa pia kuamni kwamba walioenda kutekeleza hiyo amri walikuwa polisi na mkuu wao sijui alikuwa Omar Mahita au nani vile?

Katika mojawapo ya mafundisho makuu ya imani ya Uislam ni Kumwamini na kumtii Mwenyezi Mungu Mmoja na Mtume wake Mohammed SAW, na kwamba maelekezo na sharia za Mwenyezi Mungu ziko juu ya maelekezo ya binadamu. Naamini pia kuwa Waislamu wanapata mafundisho ya imani tangu wakiwa watoto wadogo. Nadhani katika madhehebu ninayoyajua Waislamu ndiyo wako makini zaidi kuwafundisha na kuwalea watoto wao kuifahamu kuruani vizuri na nguzo kuu za imani ya Kiislam.

Kama viongozi wa serikali miongoni mwao ni waislam, pole umesema ni wachache (kwa kweli mimi sijawahi kuwahesabu japo walau sasa tuna Rais, Makamu, Mkuu wa Jeshi la polisi, Mkuu wa usalama wa Taifa, Jaji Mkuu, Mkuu wa mkoa wa Dar Es salaam, Mkuu wa mkoa wa Pwani, Waziri ofisi ya Rais Utumishi n.k sina uhakika na dini zao lakini walau kwa kutumia majina) na wamefundishwa wakaiva kutii imani yao kikamilifu iweje leo waamrishwe na Padri Camilus kuua waumini wenza kisha wakubali kutii amri ya kipuuzi namna hiyo?

Je walifundishwa Uislam wakauelewa kweli? Hivi Muislamu wa kweli na siyo wa Jina akipewa uchaguzi kati ya kumtii Mwenyezi Mungu au kutii maelekezo ya binadamu yanayopingana na maelekezo ya Mungu atachagua kipi? Je, ataakubali kukanyaga amri ya Mungu ili atekeleze ya binadamu? Huyo kweli tutamuita Muislamu kwa imani au Muislamu kwa jina tu?

Mimi binafsi sikatai unachokisema sina ushahidi nadhani na wewe pia huna ushahidi unaoweza kuutoa ukakubalika kidini na kimahakama kwamba kweli Huyo Padri Camilius alitoa amri ya kuua waislamu na kweli Maraisi wetu wemekubali kutekeleza hiyo amri. Kama hatuna ushahidi dini zote zinatukataza kushuhudia kitu ambacho hatuna ushahidi (wa kuona, kusikia kwa masikio yetu, kuonja nk.), mafundisho ya dini yanatukataza kabisa kufanya hivyo.

Lakini langu si kutilia mashaka ushahidi wako bali ni kutilia mashaka imani za hawa viongozi wa serikali walio waumini wa Uislamu. Kwamba wanaweza kukubali kutii maagizo ya binadamu tena yanayowataka waue waumini wenzao halafu wanakwenda kutekeleza kama wajinga fulani. Kwa kanuni ya imani ya kiislamu Mungu anakutaka ulinde imani yako hata kama itabidi ufe. Hainiingia akilini kwamba Muislamu wa kweli anaweza saliti imani yake kiasi hiki.

Maana yake nini basi? Maana yake ni kwamba hawa viongozi walioko serikani tena wakishika nafazi nyeti basi sio Waislam na tazizo kubwa ni wao wenyewe.

Sidhani kama hiyo ni sawa. Nawaheshimu sana viongozi wetu kibinadamu nawaona ni Waumini wa kweli, wanatii nguzo zote za imani ya Kiislamu na haiwezekani wate wakakubali kumtii huyu Padri na kusimamia kuua waislamu wenzao. Nadhani tunahitaji kuchambua ushahidi ulioutoa una walakini. Baadhi ya viongozi wa dini (zote) imeonekana mara nyingi wakitoa maneno yao na kupotosha hata maandiko matakatifu. Mfano mzuri tuliousikia juzi kule Geita kwamba Muhubiri kanisani kafundisha eti Waislamu wakichinja mnyama wanafanya ibada ya miungu yao, hiyo si kweli hata kidogo (waislamu hawaabudu miungu wanaabudu Mungu Mmoja hilo liko wazi hata kwenye Quran). Lakini lilifurahisha waumini wakaja na uamuzi basi hawatakula nyama ya manyama aliyechinjwa na Muislam. Imetokea shida tuijadili siku nyingine. Kwa mantiki hiyo hiyo ushahidi wa prof Hamza Njozi una mashaka pia. Hata kwa nchi zinazoendeshwa kwa Sharia huuwezi kuutumia kuhukumu kwa haki. Hata kidogo. Kuna viongozi wa dini wanataka umaarufu ‘popularity’ bila kujali gharama.

Nashauri tu kwamba Tanzania ni nchi yetu sote Waislam, Wakristo, Wahindu, Wayehova, Freemasons, Waumini wa dini za asili, na wasio na imani yoyote hapa ni kwetu, nakumbuka mzee Mwinyi alisema ‘Ruksa’. Tukubaliane tuishi kwa imani maisha yenyewe yakiwa marefu ni miaka 70 tunaondoka. Maendeleo ya maisha yetu hayataletwa na viongozi na wanasiasa yataletwa na sisi wenyewe. Kila mmoja akipigana kuushinda umaskini, ujinga na maradhi. Tutagombania urais, rais ni mtu mmoja kwa kila miaka mitano na saa zingine tukimpenda miaka kumi. Watanzania tuko million 45 sasa, ni upumbavu kupigania nafasi hii moja. Ndani ya maisha yetu tuna nafasi nyingi tu za kung’aa tuzifanyie kazi hizi. Tunahitajiana sana. hata tukiipa dini moja serikali nzima viongozi hawafiki hata 1,000, sie bado tuko 44,999,000 kazi yetu ni kuwadai watumie kodi zetu vizuri. Tukigombana sisi kwa sisi wao watafaidi ni marafiki hawa sie ndo tutaumia. Mali za umma zinafujwa hatuhoji, watoto wetu wamefeli hatuhoji, mahospitalini hakuna dawa, vitanda nk hatuhoji. Maji safi na salama ya kunywa shida hatuhoji. Hii ndiyo kazi yetu bila kujali aliyeko hao ni Mpagani, Muislam, Mkiristo, Myahudi, Muyunani wala yeyote. Shida yetu ni ilani ya uchaguzi tu. Misahafu ni kwenye nyumba za ibada.

Viongozi wa dini waache kuchochea ugomvi wa kidini. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Waache kutoa matamko, tuitake serikali ilinde wananchi wote na kuwatendea wote haki.

Tuache hizi conspiracy theory, ikitokea vita ya kidini Tanzania hakuna mshindi. Kwa nini tunataka tuende huko?

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

What’s this?

You are currently reading Je, viongozi wa serikali wanaweza kupewa maelekezo na kiongozi wa dini fulani kuua waumini wa dini nyingine? #ChangeTanzania at kadulyu.

meta

%d bloggers like this: