Je, viongozi wa serikali wanaweza kupewa maelekezo na kiongozi wa dini fulani kuua waumini wa dini nyingine? #ChangeTanzania
February 22, 2013 § Leave a comment
Kuna mjadala unaoendelea kuhusu misuguano ya kidini na hasa imeanzia wapi unaoendelea kwenye blog ya #ChangeTanzania.
Ndugu Aballah aliandika kwamba kuna padri mmoja kwa jina la Padri Camilius aliwahi kutoa amri ya kuua waislam na serikali imekubali kutekeleza amri hiyo. Anasema hayo yameandikwa katika kitabu Kilichoandikwa na Prof Hamza Njozi na anadhani ni ushahidi wa kweli. Kwanza mimi nilikuwa-shocked na habari hizi kwamba kiongozi wa dini fulani anaweza kuipa Amri serikali ikatekeleza tena ya kuua waumini wa dini nyingine. Haya ni baadhi ya maoni yangu kama una Muda yapitie. Tamaa yangu ni kuona Watanzania bila kujali tofauti zetu tunaishi kwa amani, letu likiwa moja tu kuwadai viongozi wetu wa serikali watumie kodi zetu vizuri kusukuma maendeleo lakini sisi pia tukichukua nafasi kila mmoja kwa juhudi zake kuushinda umaskini. Endelea….
Ndugu Abdallah,
Inaonekana huyo Padri Camillius Lwambano wa Kanisa Katoliki ni mtu powerful sana na wa kuogopa. Yaani anaweza kwenda ikulu akatoa amri kwamba waislamu wauawe na rais tuliyemchagua akatii amri ya Padri. Kama maneno haya ni kweli basi nchi hii ni janga.
Nasukumwa pia kuamni kwamba walioenda kutekeleza hiyo amri walikuwa polisi na mkuu wao sijui alikuwa Omar Mahita au nani vile?
Katika mojawapo ya mafundisho makuu ya imani ya Uislam ni Kumwamini na kumtii Mwenyezi Mungu Mmoja na Mtume wake Mohammed SAW, na kwamba maelekezo na sharia za Mwenyezi Mungu ziko juu ya maelekezo ya binadamu. Naamini pia kuwa Waislamu wanapata mafundisho ya imani tangu wakiwa watoto wadogo. Nadhani katika madhehebu ninayoyajua Waislamu ndiyo wako makini zaidi kuwafundisha na kuwalea watoto wao kuifahamu kuruani vizuri na nguzo kuu za imani ya Kiislam.
Kama viongozi wa serikali miongoni mwao ni waislam, pole umesema ni wachache (kwa kweli mimi sijawahi kuwahesabu japo walau sasa tuna Rais, Makamu, Mkuu wa Jeshi la polisi, Mkuu wa usalama wa Taifa, Jaji Mkuu, Mkuu wa mkoa wa Dar Es salaam, Mkuu wa mkoa wa Pwani, Waziri ofisi ya Rais Utumishi n.k sina uhakika na dini zao lakini walau kwa kutumia majina) na wamefundishwa wakaiva kutii imani yao kikamilifu iweje leo waamrishwe na Padri Camilus kuua waumini wenza kisha wakubali kutii amri ya kipuuzi namna hiyo?
Je walifundishwa Uislam wakauelewa kweli? Hivi Muislamu wa kweli na siyo wa Jina akipewa uchaguzi kati ya kumtii Mwenyezi Mungu au kutii maelekezo ya binadamu yanayopingana na maelekezo ya Mungu atachagua kipi? Je, ataakubali kukanyaga amri ya Mungu ili atekeleze ya binadamu? Huyo kweli tutamuita Muislamu kwa imani au Muislamu kwa jina tu?
Mimi binafsi sikatai unachokisema sina ushahidi nadhani na wewe pia huna ushahidi unaoweza kuutoa ukakubalika kidini na kimahakama kwamba kweli Huyo Padri Camilius alitoa amri ya kuua waislamu na kweli Maraisi wetu wemekubali kutekeleza hiyo amri. Kama hatuna ushahidi dini zote zinatukataza kushuhudia kitu ambacho hatuna ushahidi (wa kuona, kusikia kwa masikio yetu, kuonja nk.), mafundisho ya dini yanatukataza kabisa kufanya hivyo.
Lakini langu si kutilia mashaka ushahidi wako bali ni kutilia mashaka imani za hawa viongozi wa serikali walio waumini wa Uislamu. Kwamba wanaweza kukubali kutii maagizo ya binadamu tena yanayowataka waue waumini wenzao halafu wanakwenda kutekeleza kama wajinga fulani. Kwa kanuni ya imani ya kiislamu Mungu anakutaka ulinde imani yako hata kama itabidi ufe. Hainiingia akilini kwamba Muislamu wa kweli anaweza saliti imani yake kiasi hiki.
Maana yake nini basi? Maana yake ni kwamba hawa viongozi walioko serikani tena wakishika nafazi nyeti basi sio Waislam na tazizo kubwa ni wao wenyewe.
Sidhani kama hiyo ni sawa. Nawaheshimu sana viongozi wetu kibinadamu nawaona ni Waumini wa kweli, wanatii nguzo zote za imani ya Kiislamu na haiwezekani wate wakakubali kumtii huyu Padri na kusimamia kuua waislamu wenzao. Nadhani tunahitaji kuchambua ushahidi ulioutoa una walakini. Baadhi ya viongozi wa dini (zote) imeonekana mara nyingi wakitoa maneno yao na kupotosha hata maandiko matakatifu. Mfano mzuri tuliousikia juzi kule Geita kwamba Muhubiri kanisani kafundisha eti Waislamu wakichinja mnyama wanafanya ibada ya miungu yao, hiyo si kweli hata kidogo (waislamu hawaabudu miungu wanaabudu Mungu Mmoja hilo liko wazi hata kwenye Quran). Lakini lilifurahisha waumini wakaja na uamuzi basi hawatakula nyama ya manyama aliyechinjwa na Muislam. Imetokea shida tuijadili siku nyingine. Kwa mantiki hiyo hiyo ushahidi wa prof Hamza Njozi una mashaka pia. Hata kwa nchi zinazoendeshwa kwa Sharia huuwezi kuutumia kuhukumu kwa haki. Hata kidogo. Kuna viongozi wa dini wanataka umaarufu ‘popularity’ bila kujali gharama.
Nashauri tu kwamba Tanzania ni nchi yetu sote Waislam, Wakristo, Wahindu, Wayehova, Freemasons, Waumini wa dini za asili, na wasio na imani yoyote hapa ni kwetu, nakumbuka mzee Mwinyi alisema ‘Ruksa’. Tukubaliane tuishi kwa imani maisha yenyewe yakiwa marefu ni miaka 70 tunaondoka. Maendeleo ya maisha yetu hayataletwa na viongozi na wanasiasa yataletwa na sisi wenyewe. Kila mmoja akipigana kuushinda umaskini, ujinga na maradhi. Tutagombania urais, rais ni mtu mmoja kwa kila miaka mitano na saa zingine tukimpenda miaka kumi. Watanzania tuko million 45 sasa, ni upumbavu kupigania nafasi hii moja. Ndani ya maisha yetu tuna nafasi nyingi tu za kung’aa tuzifanyie kazi hizi. Tunahitajiana sana. hata tukiipa dini moja serikali nzima viongozi hawafiki hata 1,000, sie bado tuko 44,999,000 kazi yetu ni kuwadai watumie kodi zetu vizuri. Tukigombana sisi kwa sisi wao watafaidi ni marafiki hawa sie ndo tutaumia. Mali za umma zinafujwa hatuhoji, watoto wetu wamefeli hatuhoji, mahospitalini hakuna dawa, vitanda nk hatuhoji. Maji safi na salama ya kunywa shida hatuhoji. Hii ndiyo kazi yetu bila kujali aliyeko hao ni Mpagani, Muislam, Mkiristo, Myahudi, Muyunani wala yeyote. Shida yetu ni ilani ya uchaguzi tu. Misahafu ni kwenye nyumba za ibada.
Viongozi wa dini waache kuchochea ugomvi wa kidini. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Waache kutoa matamko, tuitake serikali ilinde wananchi wote na kuwatendea wote haki.
Tuache hizi conspiracy theory, ikitokea vita ya kidini Tanzania hakuna mshindi. Kwa nini tunataka tuende huko?
Adhabu ya jino kwa jino na Musitakabali wa imani zetu
February 19, 2013 § Leave a comment
Nabii Musa alipotoka mlima Sinai kupewa amri kumi za Mungu zilizoko kwenye kitabu cha Kutoka 20:1 – 17, Mungu alimpa na sharia zingine ambazo lengo lake lilikuwa kumsaidia kutawala na kuamua kesi za kiraia za wana wa Israel na pia sharia za vyakula.
Kwa hiyo Mungu alimpa Musa sharia za aina nne. Naomba katika kueleweshana tupitie makundi haya manne ya sharia ambazo Mungu alimpa Musa, maana yake na utekelezaji wake. Muda si punde nitaitafsiri makala hii kwa kiingereza pia ili wale ambao hawataelewa kiswahili kwa ufasaha waisome kwa kiingereza. Mungu Mwenyezi akubariki na kukulinda unapotumia muda kuelewa mambo haya na jinsi ambavyo watu wetu wamekuwa wakielewa pengine isivyo. Bofya hapo chini kupata makala yote.
When Prophet Moses went to the top of mount Sinai God did not only give him the ten commandments (the moral law) written in the book of Exodus 20:1 – 17, but also gave him other sets of laws including civil laws, ceremonial laws and dietary laws. In the essence God gave to Moses four sets of laws. To educate ourselves let’s revisit these category of laws which God gave to Moses, their interpretation, how they were meant to be implemented, which ones are still applicable to our time and which ones are no longer required.
My article is written in Swahili I’ll in a while translate it into English as well for those of you who can’t fluently follow. I advance my apology for the difficulties you may encounter. May the Almighty bless you and protect you as you take time to understand these things and where our people are getting it wrong.
Fungua hapa tafadhali: Adhabu ya jino kwa jino na Msitakabli wa imani zetu
You can start your own business now, We can all make it at some point
February 1, 2013 § Leave a comment
You can follow good tips on Wikihow. I have tried the principles and they make lots of sense. Please do.
http://www.wikihow.com/Become-a-Millionaire