Rais wetu ni mchapa kazi kwelikweli na anajitoa: Wasaidizi wake, wanasiasa mloko madarakani na wananchi tunafanyaje?

January 14, 2013 § 1 Comment

 Hamisi Kigwangalla uko sahihi ndugu yangu. JK kama mtu binafsi ni mchapa kazi kwa kweli na watanzania tunamheshimu kwa hilo. Lakini saa zingine katika nguvu zetu ndio udhaifu huonekana, katika asali kuna utamu lakini pia kuna uchungu. Nchi yetu ni kubwa sana na Rais wetu kama ulivyosema amekuwa akisimama hata pasipo na ratiba ili kutatua kero za wananchi. Swali ni kwamba ili kero zitatulike ni kweli tunamhitaji ndugu yetu apite kila mahali? Mh Rais atamaliza muda wake bila kufika kijijini kwetu nilipozaliwa. Miaka 25 ya utawala wa Nyerere hakuwahi kufika, miaka 10 ya Mwinyi hakuwahi kufika, miaka kumi ya Mkapa hakuwahi kufika, Kikwete anaenda miaka 8 sasa hajawahi kufika si kijijini kwetu bali vijiji maelfu vya watanzania na maisha yanaendelea.
Kama viongozi wengine aliowaamini na wengine walioaminiwa na aliowaamini na kukasimu madaraka kwao hawatatenda wajibu wao, haitajalisha Raisi anasimama kwenye maeneo mangapi, safari kuelekea maendeleo itakuwa ngumu. Na mwiso kwa sababu yeye ndio kashika kijiti kama kawaida atatupiwa lawama, yeye analitambua hilo. Katika hotuba yake moja ya mwisho wa mwezi aliwahi kusema, ‘ukubwa ni jalala’. Nyinyi wabunge, na watawala kiserikali msaidieni kumrahisishia kazi Rais. Kuna wakati amekuwa akiwaweka kwenye spot watendaji, utaona jinsi wanavyojikanyaga kama injinia mmoja wa maji – akasema anahitaji milioni mia tano kufanya utafiti wa maji yako wapi wakati pale Rais mwenyewe aliona kisima kilichokosa huduma ya matengenezo ilihali maji yapo chini! Huko wilayani naona wataalamu wetu wanajifanya miungu wadogo, wakiacha tabia hizo wachape kazi Rais hatahitaji kupita kila kijiji. Ukaguzi wa CAG unatoa matokea ya kutisha jinsi fedha za umma ‘zinavyokulwa’, watendaji wetu serikali za mitaa na taasisi nyingi za umma wanakula bila kunawa mikono! Ripoti za ukaguzi wa CAG zinatisha, kurekebisha hili hadi Mh Rais apite? Tuitendee haki nchi hii ili itutendee haki. Tanzania ni mama yetu sote.
Habari ya maji mimi inanitia uchungu zaidi. Miaka kidogo ya nyuma wafadhili (sipendi sana hii approach lakini nitafanyaje baba? ndio viongozi wetu mnavyopenda) walijenga visima vingi tu kwa mipango mbalimbali ya uhisani. Vingi kati ya hivyo havifanyi kazi. Serikali kupitia wizara ya maji wamefanya mapping ya visima hivyo kujua vipi havifanyi kazi na vipi vinafananya. Ripoti haijatoka lakini kitachojitokeza ni taabu tupu hakuna nafuu. Halafu unamuuliza injinia namna ya kutatua tatizo anakwambia anahitaji millioni mia tano. Maana yake nini? maana yake ni kwamba hataki kutatua tatizo la wananchi, anaweka vigingi. Haoni hata opportunity ya kuongea na rais kwamba angetatua kero hii kwa urahisi. Visima vipo vingi vyenye maji chini lakini hakuna ukarabati unaofanywa, wilayani wanapanga kuomba fedha kubwa kubwa, wakose wapate visingizio. Hivi tatizo kweli ni Rais kupita mahali au nisisi viongozi waandamizi, wanasiasa mloko madarakani na wananchi kwa ujumla ndio tatizo. Tatizo la Tanzania wala sio kubwa kihivo hadi tumtese mheshimiwa kupita na kulala saa saba usiku kisha tutafute umaarufu rahisi wa kumsifia.
Advertisements

§ One Response to Rais wetu ni mchapa kazi kwelikweli na anajitoa: Wasaidizi wake, wanasiasa mloko madarakani na wananchi tunafanyaje?

  • There is just no advantage to installing a reverse osmosis water system with today’s technological betterments. s) are smaller than water molecules so they can. The specific technique in RO will work will be as follows: Reverse osmosis pushes the liquid through the semi-permeable membrane.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

What’s this?

You are currently reading Rais wetu ni mchapa kazi kwelikweli na anajitoa: Wasaidizi wake, wanasiasa mloko madarakani na wananchi tunafanyaje? at kadulyu.

meta

%d bloggers like this: