Gesi iliyopatikana maeneo ya Mtwara ni mali ya nani? Maoni kwa Maelezo ya Waziri wa Nishati na Madini

January 4, 2013 § Leave a comment

Namshukura sana Professor kwa maelezo ya kina. Nilishasoma maelezo yake kutoka kwenye magazeti kwa makini sana. Prof katoa maelezo mazuri sana. Ninachokiona kwenye sakata hili ni kwamba Tanzania ya leo imebadilika na viongozi wetu lazima wabadilike pia. Tunahitaji kizazi kipya cha fikra (sina maana ya vijana peke yao) kuendana na mabadiriko haya. Nampongeza sana Mh. Waziri na mwalimu wetu kwa ufafanuzi na majibu ya kina kwa hoja hii ya utumizi wa mali asili zilizoko ndani ya mipaka ya Tanzania.

Tatizo la msingi ambalo raia wengi tumekuwa tukiliona ni ‘shoddy deals’ ambazo baadhi ya watu tuliowaamini wamekuwa wakiingia na wawekezaji katika sekta mbali mbali ambazo mwisho wake waTz hatufaidiki nazo bali ‘Wawekezaji’ ndio huchukua ule tunaoita ‘Mgao we simba (hasa dume)’. Mimi binafsi nina imani na hatua ambazo Prof amekuwa akichukua tangu aingie kwenye wizara hii nyeti. Aendelee tu kurekebisha bila woga.

Matatizo ambayo kwa upeo wangu nadhani ni magumu na huenda (kwa kweli niko-pestimistic kwa hili) tukashindwa ni, moja kurejea mikataba mikubwa ya madini (GGM na Barrick) ili waTz tupate fair share na pili mikataba mibovu ya kati ya Tanesco na wafuaji umeme wanaojitegemea (IPP). Hivi ni vidonda ndugu kwa nchi yetu. Viongozi waliopita kwenye taasisi hizi walituangusha. Mimi binafsi nilishawasamehe lakini swali kuu la thamani ya ng’ombe million moja (a million dollar question) ni kwamba tutatokaje hapo?

Nikirudi kwenye ishu ya Mtwara tumefikaje hapo? Mie nadhani precedence  ya madai haya imewekwa na Zanzibar. Nikiwa mfanyakazi wa kampuni moja ya kimataifa ya mafuta, niliwahi kuhusika kwenye uchunguzi wa mafuta kule Pemba miaka hiyo na mambo mengine ambayo siwezi kuyataja katika uwanja huu. Tulichelewa kuanza jitihada za kutafuta mafuta (nadhani hata sasa bado hawajaanza), kutokana na SMZ kufikiria kwamba mafuta yatayopatikana kule Zanzibar Serikali ya Jamhuri ya Muungano haitakiwi kuhusika na mali asili hii. Binafsi nilisikitika sana. Swali lililokuwa likinisumbua (mie nimezaliwa ndani ya Muungano) ni kwamba hivi tukisema nchi ya Tanzania tuna maana gani kijiografia na ki-jeolojia? Nilijua Tanzania ni nchi yote iliyo ndani ya mipaka inayokubalika kimataifa kwamba ni Tanzania ikiwemo bara, visiwa na maji yanayozunguka. Iweje leo mali asili inayopatikana mahali fulani iwe tu ya watu walioko pale? Kama bara tunafanya hivyo ni makosa pia.

Kinachosikitisha viongozi wa juu wanaelekea kulikubali hilo kwamba mafuta yakipatikana Zanzibar basi ni ya wazanzibari tu! Does it make any political and economic sense? Umeme unaofuliwa kwa kutumia gesi hauendi Zanzibar? Mchele unaopendwa Zanzibar unatoka wapi? n.k. Nadhani ndugu Msomaji unanielewa. Hii ndiyo imeweka mfano mbaya kiasi kwamba sasa watu wa eneo fulani wanaweza kudai mali asili inayotokea pale iwafaidie wao kwanza. Watanzania bara wengi tunadhani kinachotekea Zanzibar hakituhusu, tunasema wana nini hawa! Si kweli, hii ni nchi moja hii mambo ya kuwa na serikali mbili ni sarakasi za kisiasa tu na kuwaridhisha watu kadhaa, Tanzania ni nchi moja. Asiyelikubali hilo kwa dhati atatuletea matatizo tu kama si leo basi kesho – hasa kama ni kiongozi.

WaMtwara wameona inadaika, wanaona gesi ni ya kwao siyo ya Tanzania, same as WaZanzibari walivyoona mafuta ni ya kwao siyo ya Tanzania. Tukiwakubalia basi tuweke kanuni zitakazotumika kwa nchi nzima na siyo Zanzibar tu. Mwalimu alituambia ukiruhusu ubaguzi effect zake zina-trickle down further.

Mwisho Msomaji nisikuchoshe na maelezo marefu, siyo kawaida yangu na sina utaalamu wa kuandika namna hii, penye moshi pana moto ndani yake. Maana yake nini watu wa Mtwara wametoa moshi tu lakini kwa upeo wangu nadhani tutanue mawazo yetu zaidi ya hapo kwa mfano:

1. Tunapo-exploit mali asili mahali fulani tufikirie pia kufanya vitu vitakavyogusa watu wa eneo hilo na hasa huduma za jamii (social services) kama afya, maji, elimu, miundo mbinu (barabara, mawasiliano na uchukuzi). Miunganiko ya kibiashara (linkages) na ajira.

2. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilindwe na viongozi wakuu. Wasione haya, wasitafute political correctness au umaarufu (popularity). Ukweli usimamiwe hata kama utagharimu. Kanuni kuu ni kwamba Mali asili ni mali ya Tanzania siyo ya mtu wala watu wa eneo fulani. Tuingie mikataba na wawekezaji itayolinda kanuni hii. Watanzania wote tufaidike. Kama gesi itasaidia kuzalisha umeme mwingi, itaokoa utumizi wa fedha za kigeni kama Mh. Muhongo alivyosema basi tuweke miradi ya kusambaza umeme hadi vijijini (siyo tu vya Mtwara bali vijiji vya Tanzania).

3. Matumizi ya fedha itayopatikana kutokana miradi hii mikubwa yajadiliwe kwa upana na uwazi na mwisho kanuni ya nchi yaani Watanzania wote wafaidike na matumizi hayo. Kwa mawazo yangu, mapato ziada yatumike kuimarisha huduma za jamii. Kwa nini? kwa sababu huduma za jamii hugusa kila mtu na husaidia kuwapatia wananchi uwezo (wale wenye bidii na kujituma) wa kujikwamua kiuchumi.

4. Iwe mwiko tena kuingia shoddy deals na wawekezaji. Gas imebadili Qatar kwanini isiwe Tanzania (including Mtwara of course). Faida na matumizi ya fedha zitakazopatikana kutoka kwenye miradi ya namna hii (I mean all extractive industry) ijulikane itakuwa wapi na mawazo ya Watanzania wakiwemo watu wa Mtwara yazingatiwe. Pia Watz tuwe wazi na objective kuhusiana na kile tunachokitaka.

5. Maamuzi ya wapi tuweke kipi yafuate sababu za kisayansi na kiuchumi, siasa iwe tu kama icing sugar kwenye keki. Kwe mfano sitegemei mbunge atakuja na hoja kwamba dhahabu ibaki Mwanza au lazima kiwanda cha kusafisha dhahabu kiwekwe Dar. Kama kisayansi na kiuchumi ni mwafaka (convinience) kuweka Mwanza au Dar basi hizo tu ndio iwe kigezo siasa inaweza kuwa kwa mfano mmoja wa board members board ya Dhahabu (kama itakuwepo) atoke Mwanza! Ninalisema hili kwa mifano halisi. Pale Sengerema kulikuwa na Mbunge wakati fulani akavutia sana lazima kuwe na kiwanda wilayani kwake pia. Kilipokuja kiwanda cha kutengeneza wanga kwa namna fulani aka-influence kikajengwa pale Katunguru. Mali ghafi ya kiwanda ni mihogo kajenga hoja kwamba Sengerema kuna mihogo mingi sana. Kilipoanza kufanya kazi kumbe kinahitaji mihogo mingi sana, na hawa watu mihogo pia ni chakula, unategemea nini? Eneo lile walikabiliwa na njaa na kiwanda kikafa. Mfano mwingine Kilimanjaro Machine tools – hiki kilidhamiriwa kiwe kiwanda mama cha vipuri, kikajengwa Moshi pale njia panda ya kwenda Machame. Kwa influence ya nani, sijui. Hebu fikiria mali ghafi yake inatoka/inapitia Dar kisha iende Moshi halafu finished components zirudishwe kuuzwa Dar. Hayo yalikuwa maamuzi ya kiuchumi kweli. Naamini kwamba kusafirisha gesi Dar michanganuo ya kiuchumi ilifanyika na kuongoza kufanya maamuzi ya kuisafirisha Dar badala ya kujenga mitambo ya kufua umeme Mtwara kisha kuunganisha umeme kwenye grid ya Taifa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

What’s this?

You are currently reading Gesi iliyopatikana maeneo ya Mtwara ni mali ya nani? Maoni kwa Maelezo ya Waziri wa Nishati na Madini at kadulyu.

meta

%d bloggers like this: