Hapo zamani za kale palikuwagepo

October 3, 2012 § 8 Comments

Hapo zamani palikuwagepo na simba aliyejulikana kama mfalme wa wanyama wote porini. Siku moja aliamua kumtembelea Sungura aliye julikana kuwa mwerevu na mjanja sana kule porini. Basi, simba alipofika nyumbani kwa Sungura mjanja, sungura akatoka akamkaribisha akae. Simba akakataa kukaka akamwambia,’ mie nina njaa kweli sijala siku ya tatu sasa, Swala na nyumbu ambao ndio chakula chetu ukoo wa kifalme wamegoma, wanasema tusubiri hadi mmoja wao afe ndio tule mzoga’. akaendelea Kumwambia sungura,  ‘mgomo huu umetushangaza sana familia ya kifalme na katika kikao chetu cha ikulu jana tumeamua kuwa kwa sababu nyie mko jirani na ni wengi basi nyie ndo mtakuwa chakula chetu’.

Sungura wakati huo alikuwa anamsikiliza kwa makini sana. Baada ya maelezo marefu kutoka kwa simba kuhusu maamuzi ya familia ya kifalme, sungura akamwambia, ‘lakini mfalme kwa nini uhangaike kutafuta chakula wakati mnazaa vitoto vingi hivyo?’, ‘Sie sungura tuko wadogo kama vile vitoto vyenu na hata nyama ya vitoto vyenu ni tamu kuliko yetu’. Simba baada ya kusikiliza kwa makini akamshukuru Sungura kwa ushauri wake akarudi nyumbani.  Alivyofika tu nyumbani akaanza kukamata vitoto vyake na kuvila, alipokuja mama wa vitoto vile akakuta vitano vimeshaliwa tayari. Simba jike akaanza kugomba na kupigana na mumewe. Baada ya ugomvi simba jike akamuuliza dume kwa nini umefanya kitendo kibaya namna hii? Simba dume akajibu, ‘ ni shauri ya sungura, kaniambia watoto wetu ni watamu kuliko wao’.

Simba jike alikasirika sana akamwendea sungura mbio, Sungura kuona hivo akatoka mkuku. Wakaanza kufukuzana hadi kwenye kichuguu, sungura akaingia kwenye shimo. Simba akakamata mkia akaanza kuvuta, Sungura alipoona kashikwa mkia akamwambia simba,’ mbona unaacha kushika mkia unashika mzizi wa mti?’. Simba kusikia hivyo akaachia mkia wa sungura akashika mzizi wa mti akidhani ndio mkia wa sungura. Sungura akamwambia shikilia hapo, vuta kwa nguvu. Sungura akajichimbia chini zaidi na simba hakuambulia kitu, akarudi nyumbani kwa huzuni.

Hadithi hii inatufundisha nini Watanzania? Inawezekana miaka yote 50 ya uhuru tumeshikilia na tunaendelea kuvuta mzizi? Kwa nini sasa tusiache mzizi labda tu kama ni mzizi wa fitina, tushike hasa ule mkia?

Ni mawazo yangu mepesi tu. Hii hadithi nilisimuliwa na babu yangu wakati nikiwa mdogo.

FLAMES OF GOSPEL FIRE

October 2, 2012 § Leave a comment

Please follow this online, found it interesting and inspiring. Helps to take you out of your busy schedule and a perfect break after the tiring traffic jams in our towns. Please enjoy the below link:

http://www.hopetv.org/watch/live-streams/international/

Where Am I?

You are currently viewing the archives for October, 2012 at kadulyu.